Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.
Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.
Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji