Waliodanganya mtihani wafukuzwa India
Wakuu wa jimbo la Bihar, India, wamewakamata mamia ya watu na wamewafukuza wanafunzi zaidi ya 750 baada ya video kutanda mtandaoni, zinazoonesha wanafunzi wakidanganya wazi kwenye mtihani wa kumaliza shule.
Baadhi ya wazee na askari polisi wamekamatwa, na mitihani ijayo katika vituo vine imeahirishwa.
Picha hizo zinaonesha wanaume wakiparamia kuta za vituo vya mitihani na kuwakabidhi wanafunzi majibu, na wanafunzi wengine wakikopi kutoka maelezo hayo.
Maoni
Chapisha Maoni