Ndege za kivita mapema leo zilishambulia ngome ya waasi wa Houthi karibu na Ikulu ya Rais wa Yemen mjini Sanaa.
Mashambulio hayo yanayoongozwa na majeshi ya Saudi Arabia yanajaribu kukomesha nguvu za kundi la waislamu WaShia-Houthi katika taifa hilo, lililoko katika rasi ya Arabian.
Shambulio jingine lilisambaratisha kabisa zana za kivita zilizokuwa katika kituo kimoja cha kijeshi.Mapema leo ijumaa alfajiri, mashambulio kadhaa kusini mwa mji mkuu Sanaa, yaliharibu kituo cha jeshi la aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Ali Abdullah Saleh, mshirika mkuu wa kundi la Houthi.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Yemen, amesema kuwa mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na Saudi Arabia dhidi ya waaasi wa Houthi, yanafaa kusitishwa mara moja.Akiongea na BBC kutoka mji wa Sharm El Sheikh, Bwana Riyadh Yasin anasema kuwa kampeini hiyo ya mashambulio yanafaa kusimamishwa katika kipindi cha siku kadhaa au hata masaa machache yajayo, ikiwa vita vya waasi wa Houthi vitasimamishwa.
Awali alisema kuwa kuwa mashambulio hayo ya angani yanatekelezwa kwa manufaa ya watu wa Yemen.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao