Rwanda:Serikali yaagizwa kuishtaki BBC
Tume ya uchunguzi nchini Rwanda imebaini kwamba kipindi cha shirika la habari la BBC kilichopeperushwa hewani na kuuliza maswali mengi kuhusu mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 hakikufikia kiwango kinachohitajika cha kitengo cha uhariri cha shirika hilo.
Kiongozi wa tume ilioanzisha uchunguzi kuhusu kipindi hicho |
Mkuu wa tume hiyo Martin Ngoga alipendekeza serikali ya Rwanda kuanzisha kesi ya jinai dhidi ya shirika hilo.
BBC imesema kuwa imesikitishwa na matokeo ya uchunguzi huo na inatathmini athari zake.
Serikali ya Rwanda ilisimamisha matangazo ya shirika la BBC kupitia huduma yake ya kinyarwanda baada ya kipindi hicho kilichopeperushwa na runinga ya BBC na kuwashtumu watayarishaji wake.
Maoni
Chapisha Maoni