Utandawazi, umasikini wa kipato katika familia na tamaa mbaya chanzo cha mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule sekondari na msingi
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bishop Mpango iliyoko Kibondo |
Utandawazi, Umasikini wa kipato katika familia, ukosefu wa
maadili ya utumishi Mila na destuli na Tamaa za vitu vidogovidogo vimetajwa
kuwa ni vyanzo vya kuwepo kwa mimba za utotoni, kwa wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari pamoja na watoto walioko mitaani.
Hayo yamesemwa na Baadhi ya Wanafunzi wa shule hizombalimbali,
Wilayani Kibondo mkoa wa kigoma, walipokuwa wakiongea na Muhingo Blog jana kwa nyakati tofauti mjini humo.
Waamesema kuwa umasikini
ni chanzo kikubwa hasa kwa wanafunzi wa shule za sekondari wakutwa kwa
kutoishi Bweni kwani muda mwingi uwa mitaani na wengine kutopata chakula na
mahitaji muhimu hali inayowapeleka katika vishawishi na kujikuta wametumbukia
katika kufanya ngono na kubeba mimba katika umri mdogo
Hata hivyo, waliweka
wazi kuwa wapo walimu ambao nao wamekuwa wakiwasumbua wanafunzi mashuleni kwa
kutaka wafanyenao mapenzi nakuwalagai kwa kuwapa vitu vidogovidogo na hatimae
kuwapachika ujauzito, ikiwa ni pamoja na utandawazi kama wanavyoeleza Lidia Ladslaus na Enock Arcado wanafunzi.
Walieleza kuwa wapo
baadhi ya watumishi wa afya ambao ufanya kazi za kuwatolea mimba watoto
na kusababisha kutokuwepo na hofu miongoni mwao japo ni hatari kwa maisha yao huku baadhi ya wanafamilia
kutengeneza mahusiano ya kindugu kwa kuwalazimisha vijana wao hata kama wana
umri mdogo kuwaoza pasipo kujali kama
wanasoma shule walieleza Hadija Shija na
Nomi Maulidi wanafunzi wa Bishop
Mpango shule ya sekondari
Helieth Samweli, ni mwalimu katika shule ya sekondari ya
Mpango, alisema kuwa lipo tatizo kwa walimu ambao wanaajiliwa wakiwa na umri
mdogo ambapo wanapofika mashuleni ujikuta wanaanzisha mahusiano ya kimapenzi na
wanafunzi hali ambayo uchangia kushuka kwa kiwango cha elimu na mimba za
utotoni, huku mwalimu Chizero Bungubuliho, ambaye mkuu wa shule ya
Maragalasi anasema kuwa wanafunzi
wanaobeba ujauzito kwa kiwango kikubwa ni wale wakutwa kwasababu ukaa muda
mwingi mitaani tofauti na wale wa Bweni
Nae Afisa Elimu wa shule za Sekondari wilayani kibondo Bi, Honoratha
Kabundugulu, amekili kuwepo kwa tatizo la baadhi ya walimu kufanya mapenzi na
watoto wa shule, hatua aliyoitaja kuwa
chanzo ni tatizo la ajira, hivyo vijana
wengi uingia katika taaluma ya ualimu
bila kufuata maadili ya kazi na kuwafanya maafisa elimu badala ya kuwalea
wanafunzi, ugeuka na kuwa walezi wa walimu.
Mmoja wa wazazi Bw, Julias Bunyambo, mkazi wa kibondo alikataa
malalamiko ya watoto hao si sahihi kwani kipindi hiki watoto wengi wanakumbwa
na mmomonyoko wa maadili na kuwa na tamaa zisizokuwa za msingi hata kama
wanapatiwa huduma zote na kuwataka
kuwa kwani yeye anawatoto wa kike ambao
amekuwa akiwapa huduma zote lakini walibeba ujauzito mashule na sasa anafanya
kazi ya kulea wajukuuna mama zao, na kuwataka wanafunzi watulivu na kuvumilia hadi watimize
ndoto zao kwani hata watu wazamani walisoma .
Blog hii, ilifika katika Hospitali ya wilaya ya Kibondo na
kuongea na Mratibu wa Afya ya uzazi wa wilaya Bi Edna Lymo ambaye anaeleza kuwa
kumekuwepo na changamoto ya mimba za utotoni lakini tatizo kubwa kutokuwepo na
uelewa katika jamii na watoto wenyewe juu ya afya ya uzazi kwa sababu wizara ya
Afya na wizara ya Elimu hawajakaa pamoja na kuweka utaratibu ili elimu ya afya
ya uzazi ifundishwe mashuleni kwa kuhofu kuwepo uharibifu mkubwa.
Wilaya ya Kibondo tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2014 hadi
sasa imekuwa na wanafunzi watoro wa kudumu hasa kwa shule za msingi
wapatao 2800 ambapo wanaobeba ujauzito
uamua kutoroka kabla kabainika na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni