Wanajeshi watoto waachiliwa Sudan Kusini

Waasi nchini Sudan Kusini wamewaachilia huru wanajeshi watoto wapatao 250 .
Ni oparesheni ya tatu katika msururu wa hatua zilizoanza kuchukuliwa na jeshi hilo mnamo mwezi Januari.
Mpango huo unatokana na makubaliano ya amani yaliotiwa sahihi mwaka uliopita kati ya serikali na waasi katika jimbo la Jonglei wanaojulikana kama Kobra.
Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF ambalo linasaidia katika operesheni hiyo limesema kuwa watoto wengine 400 zaidi pia wataachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo na kuifanya kuwa idadi kubwa ya watoto wanajeshi walioachiliwa kufikia sasa.
Hatahivyo UNICEF limesema kuwa kuna takriban wanajeshi watoto 12,000 wanaohusishwa na mzozo unaondelea kati ya serikali na waasi wanaoungozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Wanajeshi watoto

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao