Kiwango cha Elimu hakipandi mkoani Kigoma kwa muda mrefu
Mkoa wa Kigoma umekuwa ukifanya vibaya kaika Mitihani ya
Darasa la saba kwa kushika nafasi ya 24 kati ya mikoa 25 kwa kupiga hatua ya
asilimia 1 tu na ushindi wa asilimia 42 hali iliyotajwa kuwa ni mbaya katika
ukuaji wa kiwango cha Elimu
Madiwani hao wametaja
baadhi ya mambo yanayosababisha kuwa ni pamoja na Walimu kuchelewa kufika
makazini,Baadhi ya walimu kuchelewa kutoka likizoni,Wanafunzi kutokuwa na
maandalizi ya kutosha kabla ya kuingia madarasani, ulevi wa kupindukia, mwamko
mdogo wa jamii katika elimu na Baadhi ya Walimu wa muda mrefu makazini
kuwatishia maisha waratibu elimu wa kata mbalimbali mara wanapotakiwa kufanya
ukaguzi katika maeneo yao ya kazi
Afisa elimu wa wilaya hiyo, Joseph Tirutangwa amekana kuwa
waratibu elimu wa kata haleti taarifa zilizo sahihi kwa sababu ya kutishiwa
maisha na baadhi ya wlimu ila kinachotakiwa kwa madiwani hao kufika katika
ofisi za elimu na kupata ufafanuzi wa yale wanayokuwa nawasiwasi nayo ila kwa
swala la kushuka kwa elimu hiyo ni Historia ya wilaya hiyo na siyo kwa sasa
maana nyakati maafisa elimu wote wilayani humo wanasambaa vijijini ili kufanya
ukaguzi na kuona hali halisi ilivyo
]
Hata hivyo Tirutangwa amedai kuwa ushindi wa asilimia
42% wa mkoa wa Kigoma siyo mzuri
ila kinachotakiwa ni jamii wazazi na
Walimu kushirikiana kwa pamoja ili kuinua kiwango cha elimu na pia
hawatakiwi kukata tama na wao najaribu kuwapa stahiki zao kwa wakati jinsi
serikali inavyoleta fedha
Kwa upande wao baadhi ya walimu wamekataa kuwepo kwa swala la kuwatishia Maisha waratibu elimu mara
wanapofika kwenye kazi vyao vya kazi kukangalia uendaji wao wa kazi kama taratibu zinavyoelekeza kama
anavyoeleza Edward
Buhanza shule ya Msingi Kibondo
kuwa jambo hilo hata kama lingekuwepo, haliwezi kusabisha kushuka kwa kiwango
cha Elimu
Aidha amesema kuwa mambo yanayochangia kushuka kiwango cha
elimu ni pamoja Walimu kuwa na Mikopo
yenye riba kubwa, ambayo inawafanya walimu wengi kushindwa kufanya kazi bidii, Moyo wa kufundisha kwa kujitoa kwa
walimu umeshuka kwa kiasi kikubwa na
Fedha za kuendeshea shule kuchelewa na
zikiletwa uwa ndogo hivyo kutokidhi mahitaji kwa sababu walimu ukosa vifaa vya
kundishia na kujifunzia
Kwa upande wao baadhi ya walimu walipoulizwa kwanini upenda
kujiingiza kwenye mikopo ya ri kubwa na kushindwa kufanya kazi walioajiriwa
kwayo, wameeleza kuwa ni kulingana hali ya maisha ilivyo kwa hivi sasa ikilinganishwa na mishahara ilivyo kama
anavyoeleza mwalimu Anna Maulidi toka shule ya msingi Mapinduzi japo anasema
kuwa kwa hivi sasa yeye shuleni kwao walianzisha saccos ya shule hivyo jambo
hilo haliwaahiri sana
Nae mwanafunzi Lidia Dickson ambaye ni mwanafuzi wa shule ya
msingi Mapinduzi aneleza maandalizi yake anayokuwanayo kabla na baada ya kwenda
shule na jinsi anavyoimizwa na wazazi
wake kujali masomo kuwa ndo msingi na mwanga wa maisha yake ya baadae
Wananchi wameiomba idara ya elimu ya wilaya hiyo kuhakikisha
inaweka usimamizi mzuri kwa kuwa muda mrefu yamekuwepo malalmiko kuwa usimamizi
wake hauridhishi ndo sababu wanafunzi wakuwa wakishindwa mara kwa mara kwenye
mitihani yao kama anavyoeleza Falesi Magwala mkazi wa Kibondo
Idara ya elimu ilikuwa na wanafunzi ambao ni watoro wa
kudumu wapatao 2800 kuanzia mwezi october
mwaka jana katika shule za msingi
na wengi wao uacha masomo na kukimbilia wilayani urambo mkoani Tabora kufanya
kazi katika mashamba ya Tumbaku, wengine ukimbilia wilayani Kahama mkoani
Shinyanga kufanya kazi za kuchota maji na kuchunga Ng’ombe
Maoni
Chapisha Maoni