Kamati ya Bunge yaitia Kiti Moto Halmashauri ya Wilaya Kibondo
Selemani Zed makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge |
Kamati ya Bunge yaitia Kiti Moto
Halmasauri ya Wilaya Kibondo
Kibondo,
Kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa imeeleza kutoridhishwa na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi ya Halmashauri ya wilaya Kibondo
mkoani Kigoma, kutokana na kuwepo mianya mingi inayoashiria ubadhirifu wa fedha
za miradi.
Akitoa majumuisho ya maoni ya wajumbe wa kamati hiyo Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Suleiman Zedi ameitaka Halmashauri kutoa taarifa za
kina na kuziwasilisha kwa mkaguzi na mdhibiti wa serikali Kigoma ambao
wataipatia kamati hiyo taarifa hiyo.
Wakati wa majumuisho yake kwa kamati Mwenyekiti huyo, Zed amesema
kuwa kamati imeshangazwa na kitendo cha Halmashauri kushindwa kufunga vifaa vya
kusukuma maji kwa zaidi ya miaka 5 wakati vifaa hivyo vipo,kushindwa kuweka
chujio la maji na kufanya wananchi wa Kibondo mjini kunywa maji machafu hali
ambayo ni hatari kwa afya za binadamu.
Sambamba na hilo Kamati hiyo imeshangazwa na kitendo cha
wataalam na wakuu wa idara kutumia kiasi cha shilingi milioni 80 kujilipa posho
katika mradi wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji Nyendara huku Halmashauri
ikishindwa kujenga mfereji wa kupeleka maji katika mashamba ya wakulima kinyume
na malengo yaliyokuwepo. Wakati mradi umegharimu kiasi cha shilingi
milioni zaidi ya 600 Halmashauri ya
wilaya ya kibondo imetumia kiasi cha shilingi milioni tatu tu kuchangia katika
utekelezaji wa mradi huo.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Kangi Lugora, amedai kuwa wa
Halmashauri haikuwa makini katika matumizi ya fedha za utekelezaji wa mradi huo
na kutoa mwanya wa wakuu wa idara na wataalam kujinufaisha ni pamoja na kuwepo wakuu
wa idara wakijipa kazi ya kutekeleza mradi huo badala ya kuteua kampuni ya
ukandarisi,na malipo ya zaidi ya shilingi 600,000 kwa mtoto mchanga wa mmoja wa
watumishi wa Halmashauri hiyo ambaye aliambatana na mama yake kwenye ziara za
kikazi.
Katika majibu yao kwa
kamati hiyo wakuu wa idara na wataalam wa Halmashauri hiyo wamekuwa wakishindwa
kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusiana na matumizi ya fedha za miradi huku
wananchi wakishindwa kupata huduma.
Akitoa maelezo kwa kamati hiyo,Kaimu Mhandisi wa maji wa
wilaya ya Kibondo,Tandali Matwiga alisema kuwa walilazimika kutekeleza mradi
wao wenyewe kutokana na uharaka wa mradi kwa vile wananchi walikuwa na tatizo
kubwa la maji. Huku akishindwa kuwa na maelezo ya kutosha ya kushindwa kufungwa
kwa mota na pampu kwa ajili ya kusukuma maji kupeleka kwa wananchi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Emili Mpfanye
katika kujitetea kwake aliweka wazi kuwa matatito mengi yalitokea wakati wa
uongozi uliopita na hadi ukabadilishwa akashika ngazi yeye, pia na wakuu wa
idara walio wengi ni wageni. huku Katibu Tawala serikali za mitaa mkoa wa
kigoma Moses Msuluzya akiahidi mbele ya kamati kuwa karibu na Halmashauri hiyo
ili kuhakikisha mapungufu yaliyobainika yanarekebishwa
Hata hivyo baadhi ya wananchi walipoona kamati hiyo ikikagua
chanzo cha maji cha Mgoboka walifika huku Benard Kasuka mkazi wa kijiji cha
Kumhama akitoa malalamiko yao juu ya kulipwa fidia ya mazao na mashamba ili
waweze kupisha katika eneo hilo na uendelezaji wake uweze kukamilika
walikataliwa na kuambiwa hakuna malipo kwani huo ni uhabifurifu, na serikali
ilishapiga marufuku kuendesha shuguli za kilimo katika vyanzo vya maji.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni