Wanawake Kibondo, jiepusheni na kurubuniwa na vitu vidogovidogo katika uchaguzi 2015
Wito umetolewa kwa madhehebu yote kuendelea kuliombea taifa
hasa wakati huu wa uchaguzi ambapo vitendo vya kikatili hasa mauaji ya albino
vinavyo jitokeza kwa imani za kishilikina.
Kauli hiyo, imetolewa na Bi Juster Paulo mkazi wa Urambo
mkoani Tabora, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya maombi
kwa wananwake duniani ambayo yaliandaliwa na umoja wa wananwake CCT Wilaya ya
Kibondo mkoani kigoma, kwa lengo la kuungana pamoja na kuliombea taifa, ambayo
yalifanyika jana katika Kanisa la Kiijili la Kiluthel Tanzania KKKT .
Bi. Juster amesma
viongozi wanao wania nyazifa mbalimbali ndani ya serikali wanatajwa kujihusisha
na imani za kishilikina ambapo kila ikariibiapo muda wa uchaguzi hujitokeza
mauaji ya albino na hivyo Wakristo na watanzania wote hawana budi kuungana na kuliombea taifa dhidi
ya mauaji hayo.
Aidha amewataka wanawake kote nchini kuacha tabia ya
kuendekeza kupewa viu vidogovidogo na baadhi watu wanaogombea nafasi mbalimbali
ili waweze kuwachagua kwani hata wanawake wanahaki sawa na watu wengine hivyo
hawastaili kudharaliwa wala kujinyanyapa na wanatakiwa kujisimamia utu wao
Kwa upande wao baadhi ya akina mama wamesema ni vema
kusikiliza sera za wagombea na kuwapima kwa hotuba zao badala ya kuwa wepesi
kupokea zawadi ambazo hazina mashiko katika uongozi wa serikali ili kutengeneza
utawala bora ujao katika nchi alieleza Bi
Namsifu James mkazi wa kibondo
Siku hii ya Maombi ya Dunia
kwa Wanawake uadhimishwa kila
mwaka katika mwisho wa wiki ya kwanza ya mwezi marchi kabla ya maadhimisho wa
siku ya wanawake Duniani ambayo ufanyika mwezi march kila mwaka, ambapo umoja wa wanawake
wa CCT Kibondo wameadhimisha kwa kuliombea Taifa juu ya
uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika October mwaka uhuu uwe
wa amani kama alivyosoma lisara ya umoja huo, Bi Melse Bulugu katibu wa umoja
wa wanawake
Pamoja hayo wamesema kuwa wanawake wengi wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuachiwa mizigo mikubwa ya kulea na
kuhudumia familia na mifumo ya zamani ya wanake kutokupata nafasi ya kupaza
sauti zao kuzifanya familia kutopiga hatua katika maendeleo, hayo anayaeleza Bi
Sarah Wiliam huku wanaume wanao wakitoa maelezo yao kuwa majukumu ya Baba
katika familia hayawezi kufanya uwenda
ndo sababu wakina mama udhani wameachiwa mzigo wa familia peke yao
Sambamba na hilo katika maadhimisho hayo wakina mama hao wao
wameshiriki kutoa msahada thamani ya shilingi laki 7ikiwa ni Sabuni na Mafuta ya kupaka kwa Wafungwa na maabusu kwenye Gerza la
Wilaya Kibondo lengo iikiwa ni kuwafariji binadamu wanaoishishi katika
mazingira magumu
Maoni
Chapisha Maoni