Mashambulio Maiduguri yauwa watu 40
Mashambulio ya kujitolea mhanga yaliyofanywa kaskazini-mashariki mwa Nigeria katika mji wa Maiduguri, jimbo la Borno, yameuwa watu zaidi ya 40.
Inaripotiwa kuwa miripuko mitano imetokea katika masoko mawili na kituo cha basi.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram imezidisha mashambulio kwa sababu inaona imeandamwa na serikali.
Likisaidiwa na wanajeshi kutoka Chad, Cameroon na Niger, jeshi la Nigeria limekuwa likijaribu kuwatimua wapiganaji katika mashina yao ya kaskazini-mashariki kabla ya uchaguzi mwezi ujao.
Inasemekana kuwa mabomu hayo yaliripuliwa na wanawake waliojitolea mhanga.
Mkuu wa sheria na mahakama katika jimbo la Borno, Kaka Shehu, alisema mashambulio hayo ni ya kikatili na kishenzi.
Maoni
Chapisha Maoni