IS yataka Wanajeshi 100 wa US wauwawe

Jeshi la Marekani linasema kuwa linawajulisha karibia wanajeshi 100 waliotajwa kwenye orodha ya mtandao ulionzishwa na Islamic State unaotaka wauawe.
Kitengo cha kudukua mitandao cha Islamic State kinawataka wale wanaolipendelea kundi hilo kuwaua wale walio kwenye orodha hiyo ambao Islamic State inawalaumu kwa kuendesha mashambulizi ya angani dhidi yake nchini Iraq na Syria.
Majina yao, picha na namba zao zimechapishwa kwenye mitandao.
Kitengo cha ujasusi cha jeshi la wanamaji la Marekani kinasema kuwa tishio hilo halijathibishwa rasmi .
Kitengo hicho kinawataka wanajeshi kuchukua tahadhari kuhusu ujumbe unaowahusu wanaoweka kwenye mitandao.
Jeshi la Marekani linasema kuwa limeanza kuwajulisha wanajeshi 100 wa Marekani waliotajwa katika mtandao wa IS unaotaka wauawe

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji