Machapisho

Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini

Picha
Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini Akiongea na Wananchi wa Mikoa hiyo jana,  George Mbijima ambaye ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2016 kwenye makabidhiano ya Mwenge wa uhuru uliokuwa ukitoka Kigoma na kwenda Kagera, amewataka wakazi wa mikoa hiyo  wanapoona kuwa kuna wimbi la watu hao watoe taarifa kwa viongozi ili hatua zichukuliwe Aidha Mbijima alisema kuwa wapo baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakishirikiana na wahamiaji haramu kwa kufanya vitendo vya uharifu wa kutumia siraha kama ujambazi na ujangili hali ambayo imekuwa ikisababisha mauwaji ya raia wasiyokuwa na hatiana kirudisha nyuma maendeleo ya watu   ‘’Serikali haitalifumbia macho jambo hili na mtu yeyote atakaebainika kuwakumbatia...

Watendaji katika Idara mbalimbali za halmasauri za wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata miongozo taratibu za kazi na kutumia taalumao ili kuleta ufanisi na kuondoa manug’uniko katika jam

Picha
Kibondo ; Mkuu wa wilaya ya Kibondo Luis Peter Bule akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kasulu ulipokuwa ukianza mbio zake wilayani kibondo Watendaji katika Idara mbalimbali za halmasauri za wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata miongozo taratibu za kazi na kutumia taalumao ili kuleta ufanisi na kuondoa manug’uniko katika jamii Kauli hiyo ilitolewa jana  na Kiongozi wa mbio za mwenge  Kitaifa George Mbijima alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kibondo Mkoani kigoma mwenge huo ulipofanya mbio zake wilayani humu kama taratibu zambio  zake zinazoendelea  hapa nchini Mbijima ameseme kuwa hivi sasa serikali imeelekeza nguvu zake wanawake na Vijana katika kuwawezesha kwa kupitia katika halmashauri zao lakini wapo baadhi ya watendaji wasiokuwa waadilifu mara zinapotokea fulsa kwa walengwa wao uzipora na kuwapa watu wao au kuziingiza katika makampuni yao binafsi Mwenge  huo katika mbio zake...

Kibondo; Serikali ya Uberigiji kupitia shiraka la Maendeleo la nchini humo BTC, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania imetoa msahada wa Mahema 22 yenya thamani ya shilingi milion miamoja kwa ajili ya wakulima na wafugaji Nyuki wa Mkoa wa kigoma ili kuboresha utendaji kazi wakati wa uvunaji wa mazao ya nyuki

Picha
Mwemezi Muhingo Mwananchi Kibondo;  Serikali ya Uberigiji kupitia shiraka la Maendeleo la nchini humo BTC,  kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania imetoa msahada wa Mahema 22 yenya thamani ya shilingi milion miamoja kwa ajili ya wakulima na wafugaji Nyuki wa Mkoa wa kigoma ili kuboresha utendaji kazi wakati wa uvunaji wa mazao ya nyuki Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi mahema hayo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kigoma Kaimu katibu Tawala wa mkoa huo anaehusika na ushauri wa uchumi Robinson Mwanjala ambae alikuwa mgeni rasmi,  ameipongeza serikali ya uberigiji  wakati wa kukabidhi msahada huo na  amewataka wafugaji nyuki kuhakikisha wanayatumia ipasavyo na kwa malengo yanayo kusudiwa ili kazi yao iweze kuwa na tija Mwanjala aliwataka wafugaji hao na wakulima kuhakikisha wanatumia vizuri elimu waliopewa katika kuvuna mazao ya Nyuki kwa kuzingatia usalama wa chakula kwa watumiaji ambapo vikundi 7 vya ushirika katika wilaya za kakon...

Mkazi wa kijiji cha wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake

Picha
Mwemezi Muhingo Kibondo Mkazi wa kijiji cha Kumhama wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake Mbele ya hakimu mkazi  wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Peter Makala amemtaja mtu huyo kuwa ni Jaribu Obedi mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kumuhama wilayan kibondo Bw Makala amesema kuwa mnamo tarehe 28 mpaka 30 mwezi wa 5 mwaka huu majira ya usiku katika kijiji cha kumuhama bw Jaribu alimlawiti mkewe aitwae jina linahifadhiwa, mwenye umri wa miaka 24 akiwa na mimba ya miezi saba na kwamba alimfanyia kitendo hicho siku tatu mfurulizo Aidha kitendo hicho kilisababisha mishipa kukosa nguvu hali ambayo humsababishia kutoa haja zote mfululizo bila kujizuia wala kujitambua  hali ambayo ilisababisha dada huyo kukosa uvumilivu na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi mtaa wa migombani mjini kibo...

Serikali imeshauriwa kutengeneza utaratibu wa kuwatawanya Wakimbizi kwa kuanzisha makambi mengine zaidi katika mikoa mingine ili kuondoa mrundikano wa wakimbizi wengi katika eneo moja hatua inayosababisha kuwepo kwa uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali

Picha
Mwemezi Muhingo Kibondo Serikali imeshauriwa kutengeneza utaratibu wa kuwatawanya Wakimbizi kwa kuanzisha makambi mengine zaidi katika mikoa mingine ili kuondoa mrundikano wa wakimbizi wengi katika eneo moja  hatua inayosababisha kuwepo kwa uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali  Hayo yamesemwa na baadhi ya wadau wanaotoa  huduma kwa wakimbizi katika wilaya za kakonko na kibondo mkoani Kigoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira Duniani yaliyohusisha na utoaji  elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wakimbizi wa kambi ya Mtendeli wilayani Kakonko, kuwa ni vema makambi yakawa na idadi ndogo ya wakimbizi Nyinisaheri Gwamagobe ambaye ni Maneja wa shirika lijulikanalo kama Relief Devolment Societ REDESO, linalohisika na utunzaji wa mazingira katika makambi ya wakimbizi amesema kuwa wakimbizi wanapokuwa wengi katika eneo moja husababisha uharifu mkubwa wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo mazingira kwa muda na ku...

Kakonko;Wakazi wa wilaya ya Kakokonko mkoani kigoma wamemuomba Mkuu wa wa mkoa huo Brigedia General Msitaafu, Emmanuel Maganga kusimamia vema vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo baada ya kuingiwa na hofu kutokana na matukio ya mauwaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara

Picha
Mwemezi Muhingo, Mwananchi Add caption  Mkuu wa mkoa wa kigoma Brigedia General mstaafu akiongea na wananchi wa kakonko Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedi General a Mstaafu Emmanuel Maganga wa tatu kutoka kulia  akiwa amekaa kwenye madawati baada ya kukabidhiwa toka kwa meneja wa NMB kanda ya magharibi mjini Kakonko Kakonko; Wakazi wa wilaya ya Kakokonko mkoani kigoma wamemuomba Mkuu wa wa mkoa huo Brigedia General Msitaafu, Emmanuel Maganga kusimamia vema vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo baada ya kuingiwa na hofu kutokana na matukio ya mauwaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara Vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikifanyika katika maeneo mengi wilayani humo, watu wananyang’anywa mali zao wanajeruhiwa na wengine kuuwawa kikatili kwa kupigwa risasi na watu ambao wamekuwa hawafahamiki huku vyombo vya ulinzi vikidai vinaendelea na uchunguzi bila kutoa maelezo yanayoeleweka kwa wananchi Wakiongea jana katika kikao kilicho wahusisha viongozi wadini, ...