Kibondo;Kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake, Jamii imetakiwa kulitazama kundi hilo kwa jicho la pekee ili kuondoa kero na kuboresha maisha yao
Kibondo; Kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake, Jamii imetakiwa kulitazama kundi hilo kwa jicho la pekee ili kuondoa kero na kuboresha maisha yao Wanawake ndiyo wenye changamoto nyingi na kundi hili. liko kama vile limesahaulika lakini ndiyo wenye uthubutu katika kufanya kazi kukopa na wenye uaminifu wa kulipa fedha kama marejesho ya fedha zinazokuwa zimechukuliwa na makundi yao na kuyataka mashirika. taasisi za serikali na za binafisi kuyatazama makundi ya wanawake kwa Nyanja zote Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Juma Mnwele alipokuwa akifungua washa ya kujenga uelewa kwa maofisa ugani na waratibu elimu ili nao waweze kuwaelekeza walengwa wa mpango wa kusuru kaya kupitia shirika la Tasaf ili kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi wao kupitia shirika la hifadhi ya jamii Tasaf mafunzo hayo yanafanyika mjini Kibondo ...