Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2015

Jeshi la China laingia Sudan Kusini

Picha
Uchina imesema kuwa kikosi chake kwa kwanza maalum cha kijeshi kilichojumuishwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa kimeanza shughuli zake nchini Sudan kusini. Katika kipindi cha majuma machache yajayo, jumla ya wachina mia saba watawasili nchini humo . Watakuwa na ndege zisizokua na rubani, vifaru na makombora. Uchina haijawahi kuwatuma maelfu ya walinda amani , lakini imekuwa zaidi ikitoa misaada kwa ajili ya amani. . Ongeza kichwa

Bilioni 103 za benki ya dunia kujenga nyumba

Picha
Dar es Salaam. Benki ya Dunia (WB) imetoa Dola 60 milioni (Sh 103 bilioni) za Marekani kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wananchi. Taarifa iliyotolewa na benki hiyo, ilieleza kuwa fedha hizo zitasaidia kuendeleza mradi wa ujenzi wa nyumba ulioanzishwa mwaka 2010 na kwamba kwa sasa thamani ya uwekezaji katika mradi huo imefikia Dola 100 milioni za Marekani. Mkurugenzi wa Benki hiyo Tanzania, Burundi na Uganda, Phillipe Dongier alisema, ukuaji wa kasi wa miji unaonyesha kwamba kuna haja ya kuwapo kwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu. “Miji inakua kwa kasi, hivyo tunapaswa kutengeneza mazingira ya kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wananchi.” Pia alisema: “Lengo letu ni kusaidia upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, mpango huu utazisaidia familia zenye kipato cha chini kumiliki nyumba na kuepuka gharama za kupanga.” Dongier alisema fedha hizo zitasaidia upatikanaji wa mikopo nafuu na familia kumiliki nyumba zao badala ya kujenga nyumba...
Picha
Wakristo 21 wa madhehebu ya Coptic, raia wa Mirsi, wamekatwa vichwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu nchini Libya , lenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Picha za waumini hao ziliyorushwa kwenye mtandao zimezua hisia kali nchini Misri na ulimwengu wa Kiarabu. Kanisa la Kicoptic na Msikiti mkuu wa al-Azhar vimelani uhalifu huo wa kigaidi, wakati rais wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi, akitangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba. Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Cairo,  Alexandre Buccianti , picha ziliyorushwa kwenye mtandao zilionyesha waumini hao wa madhehebu ya Coptic wakivaa nguo za rangi ya machungwa wakikusanywa sehemu moja na watu waliokua wakivalia nguo nyeusi wakificha nyuso zao, huku wakiwalazimisha kupiga magoti karibu na bahari. Katika video hiyo Wakristo hao wameonekana wakitikisa midomo yao, ikiaminika kuwa wamekua wakifanya maombi ya mwisho, kabla ya kuchinjwa. Msemaji mmoja amesema kuwa kitendo hicho ilikua ulipizaji kisasi kwa Osama Bin ...

IS yawashikilia mateka mamia ya watu Syria

Picha
Wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu wameendesha mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa kaskazini mashariki mwa Syria, na kuwateka nyara mamia ya watu, zaidi ya 30 kuuawa na wengine kujeruhiwa. Mamia kwa maelfu ya wakazi wa vijiji hivyo wamekimbilia katika miji mikuu ya mkoa, kama Hassaké au Qamichli. Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mij wa Istanbul,  Jérôme Bastion , mapigano yamekua yakiendelea usiku wa Alhamisi Februari 26, kando ya mto Khabour ambako kunapatikana vijiji hivyo ambavyo vinakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kislamu tangu Jumatau asubuhi wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa za mwisho tulizopokea kwa simu kutoka eneo hilo, hadi watu 350 wametekwa nyara katika vijiji hivyo. Inasadikiwa kuwa watu 110 miongoni mwa wanavijiji huenda waliuawa. Kwa kweli inaaminika kuwa wanamgambo hao wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu waliwabeba wanawake na watoto katika mlima wa Abd al-Aziz, ulio karibu, ambao wameutenga kama ...

Kiev imeanza zoezi la kuondoa silaha nzito

Picha
Vikosi vya Ukraine vimeanza Ijumaa wiki hii zoezi la kuondoa silaha nzito mashariki mwa Ukraine , ambapo makubaliano ya kusitisha vita yameonekana kuheshimishwa kwa  Hatua hii ya mwanzo itachukua masaa 24 na itafuatiwa na uondoaji wa vifaa vya kurusha roketi na vifaa vingine vizito, amebaini msemaji mmoja wa jeshi alipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa   AFP . Iwapo zoezi hili litathibitishwa, itakua ni hatua ya kwanza ya uondoaji wa silaha nzito, zoezi ambalo liitaangaliwa kwa makini na jumuia ya Usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE). Kulingana na makubaliano ya Minsk 2 yaliyotiliwa saini Februari 12, zoezi la kuondoa silaha nzito lingelipaswa kuanza Jumapili iliyopita, lakini serikali ya Ukraine iliomba kwanza uheshimishwaji wa jumla wa usitishwaji wa mapigano kwa upande wa waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki. Lakini usitishwaji wa mapigano umetekelezwa kwenye uwanja wa vita. Hata hivyo, vikosi vya Kiev vimelani mwenendo wa waasi ya kuongeza idadi...

Ukosefu wa ajira unahatarisha afya za Watanzania

Picha
Wapo pia wale wanaostaafu na kujikuta hawajaandaa mazingira mazuri ya kuendelea kuwa na kipato. Hapa Tanzania ukosefu wa ajira huelezwa kuwa ni hali ya mtu kutokuwa na shughuli inayomuwezesha kupata kipato kitakachomsaidia yeye au pamoja na familia yake katika maisha ya kila siku. Kutokana na hali hiyo, wenye ajira ni pamoja na wale walioajiriwa au kuajiri kwenye mfumo rasmi au usio rasmi. Asiye na ajira anawekwa katika kundi la wale ambao hana shughuli ya kumpatia kipato. Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga alinukuliwa akisema ukosefu wa ajira kwa Tanzania umefikia kiasi cha asilimia 12. Kiasi hiki cha watu wasiokuwa na ajira ni sawa na idadi ya watu milioni sita. Watu wengi wanafikiri kuwa ukosefu wa ajira ni tatizo la kiuchumi pekee, lakini watafiti wa masuala ya afya wanabainisha kuwa hili pia ni tatizo kubwa la afya ya jamii. Katika utafiti uliochapishwa mwaka huu hivi karibuni katika Jarida la The Lancet Psychiatry, unaonyesha ...

MV Dar es Salaam yaanza majaribio, yaenda bagamoyo na kurudi Dar

Picha
Waziri wa Ujenzi Dk, John Magufuli leo amewaongoza wananchi wa jiji la Dar es Salaam kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari zake kati ya Dsm na Bagamoyo. Mamia ya wananchi wakiwa na furaha ya usafiri huo wamesafiri pamoja na Waziri Dk Magufuli bure kutoka jijini Dar hadi Bagamoyo kwenda na kurudi kujionea huduma hiyo itakayoanza kutolewa siku za usoni. Akizungumza kwenye majaribio hayo Waziri Dk Magufuli amesema lengo la Serikali kufanya hivyo ni kutaka kuharakisha maendeleo ya wananchi kwa njia yeyote akiongeza kuwa usafiri wenye tija unaongeza pato la taifa. Amesema Kivuko hicho kitazinduliwa rasmi hivi karibuni na kuanza safari zake mara moja, hivyo wasafiri wanaokwenda bagamoyo hawatalazimika tena kutumia barabara. "Mbali na kuongeza pato la taifa pia kivuko hiki kitapunguza kwa namna moja ama nyingine foleni za jiji la Dar es Salaam, amsema Magufuli. Amesema Serikali itaendelea kubuni mbinu mbalimbali za k...

Mbowe apanda kizimbani Hai, aiomba Mahakama iifute kesi yake

Picha
Hai.Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ameiomba mahakama kutupilia mbali kesi inayomkabili kwakuwa ni kesi  iliyotengenezwa  kutokana na chuki za kisiasa na jazba za kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010. Akitoa ushahidi  mbele ya Hakimu mkazi  mfawidhi  wa mahakama ya wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa ,Mbowe ameiomba mahakama kutupilia mbali kesi hiyo yenye lengo la kumpotezea muda katika uwajibikaji wake katika Taifa. Awali kabla ya kuanza kwa kesi hiyo eneo la mahakama lilijaa mamia ya wafuasi wa chama hicho kutoka  jimbo la Hai wakiongozwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho maarufu kwa jina la redbriged waliokuwa wamevalia sare na kuzingira eneo lote la mahakama . Mbowe alifika mahakamani hapo majira ya saa 14:05 ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa lakini ilishindikana na kuanza kusikilizwa majira ya saa 16:05 kutokana na uwepo wa kesi nyingine ya wananchi kuvamia shamba la mwekezaji wa...

Mchinjaji wa IS 'Jihadi John' atambuliwa

Picha
Mwanaume ambaye amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa. Bwana huyo ambaye taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza. Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi. Emnuazi ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto. Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London. Yamkini Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29 alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za kiusalama haikuwezekana kumtambua. Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo. Polisi nchini Uingereza ...

Dawa ya kupaka ili kuzuia HIV haifai

Picha
Dawa iliokisiwa kupunguza uwezekano wa mwanamke kupata virusi vya HIV wakati wa tendo la ngono haifai,kulingana na utafiti mkubwa uliofanywa na shirika la Follow on Africa Consortium for Tenofovir kutoka Afrika kusini. Matokeo ya utafiti huo unaojulikana kama facts 001 yalitolewa katika kongamano la magonjwa ya virusi na yale ya maambukizi nchini Marekani. Kulingana na gazeti la mail and Guardian nchini Afrika kusini,wanawake katika utafti huo waliagizwa kujipaka dawa hiyo katika sehemu zao za siri kabla na kila baada ya tendo la ngono. Matokeo hayo yanapinga matokeo ya utafiti mwengine uliochapishwa mwaka 2010 na shirika la mpango wa utafiti wa ugonjwa wa ukimwi nchini Afrika kusini Caprisa. Watafiti waliwatumia zaidi ya wanawake 900 katika jimbo la Kwa Zulu Natal na kuripoti dawa hiyo ya Tenofivir ilikuwa na uwezo wa asilimia 39 pekee wa kupunguza viwango vya maambukizi ya viini vya HIV miongoni mwa wanawake hao. Viwango vya maambukizi ya HIV nchini Afrika kusini vilikuw...

Waethiopia 100 wahukumiwa kifungo miezi 12 gerezani Nchini Kenya

Picha
Raia mia moja wa Ethiopia hii leo wamehukumiwa kifungo cha miezi kumi na mbili gerezani nchini Kenya au walipe faini ya takriban dola 600 baada ya kupatikana na hatia ya kuwemo Kenya kinyume na sheria. Polisi waliwakamata wahamiaji wao haramu siku ya Jumatatu katika mtaa mmoja mjini Nairobi. Maryam Dodo Abdalla anaarifu zaidi. Wahamiaji hao haramu walioonekana wachafu na waliodhoofika kwa njaa, walikiri mashtaka hayo baada ya kusomewa makosa yao mmoja baada ya mwingine na hakimu Victor Wakhumile mjini Nairobi. Sasa wanatakiwa kutumikia kifungo hicho au walipe faini waliotozwa, na baadaye watasafirishwa kurudishwa Ethiopia walikotoka. Kwa kilio, wameielezea mahakama kwamba wamewasili Kenya wakiwa wanaelekea Afrika kusini ambako wameahidiwa kupewa ajira. Polisi nchini kenya iliwanasa raia hao mia moja wa Ethiopia, mapema wiki hii wakiwa wamehifadhiwa katika chumba kimoja kidogo, eneo la Embakasi mjini Nairobi. Mkuu wa kitengo maalum cha kuzuia uhalifu nchini, SCPU, Noah Katu...

Wakristo zaidi watekwa nyara Syria

Picha
Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State. Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kazkazini mwa Syria. Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake na wazee. Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka. Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha. Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristu hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza. Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristu kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo. Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini wametekwa. Huku hayo yakiarifiwa waumii wengine wa kikristu wameanza kukimbia avijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State. Kuna hofu kuwa raia wakrist...
Picha
Jeshi la Ukraine na wawakilishi wa waasi wanaotaka kujitenga wamebadilishana wafungwa kadhaa gizani katika eneo la mapigano jana Jumamosi(21.02.2015) na kuanzisha mchakato wa kuleta amani mashariki mwa Ukraine. Wanajeshi 139 na waasi 52 walibadilishwa, kwa mujibu wa afisa wa wanaotaka kujitenga ambaye ameshuhudia hatua hiyo ya mabadilishano ya wafungwa katika eneo ambalo halidhibitiwi na upande wowote karibu na kijiji cha Zholobok, kiasi ya kilometa 20 magharibi ya mji unaoshikiliwa na waasi wa Luhansk. Basi lililojaa wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika sare za jeshi liliwasafirisha wanajeshi hao mapema siku hiyo kutoka jimbo ambalo ni ngome kuu ya waasi wa Donestk hadi katika eneo la vijijini kiasi ya kilometa 140 kaskazini mashariki , kabla ya kujiunga na makundi mengine ya wafungwa wenzao. Baada ya kuwasili katika eneo katika mji wa Zholobok , wanajeshi hao walipangwa katika mistari na kusikiliza hotuba iliyotolewa na wawakilishi wa waasi, ambao wamewaamuru watu hao kuondoka ...

Polisi watanda Muhimbili kuwazuia ‘JKT

Picha
Dar es Salaam.  Polisi wenye silaha na mabomu ya machozi pamoja na maofisa usalama, jana walitanda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuzuia vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wasimwone mwenyekiti wao, George Mgoba, aliyelazwa baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Pamoja na hatua hiyo vijana wengine watatu akiwamo katibu wa wahitimu hao walikamatwa na polisi na walikuwa wanashikiliwa katika Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam. Mgoba Jumatatu iliyopita alitekwa, kuteswa na baadaye kutupwa kichakani katika eneo la Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani. Kabla ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Muhimbili, Mgoba alilazwa kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Amana wilayani Ilala. Jana, wahitimu hao wa JKT wanaokadiriwa kufikia 200 walifika katika lango la Hospitali ya Muhimbili saa 11.50 asubuhi na kujichanganya na watu wengine waliokuwa wakisubiri kuwaona wagonjwa wao. Ilipofika saa 12.10 magar...

Pinda ammwagia sifa Peter Msigwa

Picha
Iringa.  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amemwagia sifa mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, akisema amekuwa kiongozi wa kwanza kuchangia vitanda 30 katika Hospitali ya Frelimo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Mchungaji Msigwa alimiminiwa pongezi hizo jana mchana wakati Waziri Pinda alipotembelea hospitali hiyo na kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali. Kauli hiyo ya Pinda, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, kupongeza utendaji kazi mzuri wa viongozi wanaotoka vyama vya upinzani ni nadra sana kutolewa na viongozi wa chama hicho tawala. Februari 10 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete pia alimpongeza meya wa Manispaa ya Moshi (Chadema), Jaffar Michael kwa kile alichosema ni kusimamia vizuri na kutekeleza  Ilani ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo. “Nakupongeza kwa jitihada ulizozionyesha. Kitendo ulichokifanya kinatakiwa kuigwa na wadau wengine kwa sababu hospitali hii ina changamoto nyingi, “alisema Pinda. Pinda alitaja chang...

kumi na wawili waalikwa Tanzania:magongo

Picha
Wachezaji 12 wa kriketi kutoka nchi za Pakistan, India, Afrika ya Kusini na Uingereza wawasili nchini Tanzania mwezi ujao kushiriki katika michuano maarufu ya APL T20 (kwa wanaume) inayoshirikisha wachezaji wenye kiwango cha juu. Michuano hiyo, kwa mujibu wa Afisa wa Chama Cha Kriketi Tanzania (TCA), Kazim Nasser, inaanza Machi 12 na itadumu kwa muda wa juma moja. Kila nchi itapeleka Tanzania wachezaji watatu wa kiwango cha juu watakaopendekezwa na vilabu/vyama vyao baada ya mwaliko. Kutakuwa na timu nne na kila timu itajumuisha wachezaji watatu. Wachezaji wazawa watatoka katika timu ya taifa ya wakubwa na wengine kadha wanaochipukia. Kwa mujibu wa Nasser, lengo la kualika wachezaji wanaocheza kriketi ya kulipwa (professional) ni kuwapa uzoefu wachezaji wa Tanzania na kubadilisha uzoefu. Michuano hiyo inakuja baada ya Tanzania kuandaa michuano ya vijana chini ya miaka 19 ya Afrika siku tatu zilizopita kwa ajili ya kufuzu kucheza kombe la Dunia ambapo Namibia waliibuka mabingwa...

Cannavaro aomba Watanzania kuiombea Yanga

Picha
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” amewaomba Watanzania kuiombea timu yake ili ishinde mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao, BDF XI ya Botswana. Yanga watasafiri wikii hii kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi kwanza. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam takriban wiki moja iliyopita, Yanga, ikiwa chini ya kocha Mdachi, Hans Pluijm, walishinda 2-0. “Watanzania watuombee ili tushinde na kusonga hatua ya pili”, alisema Cannavaro, baada ya Yanga kuwafunga Mbeya City 3-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara na kuongoza ligi wakiwa na pointi 31. “Mechi ya ugenini (away) mara nyingi huwa ni ngumu, tulishinda Dar es Salaam na tunahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili tusonge, Watanzania watuombee sisi na wenzetu Azam kwa sababu tunawakilisha nchi”, alisema Cannavaro. Yanga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC watakuwa na vibarua vya ugenini mwishoni mwa wiki. Azam watasafiri kwenda Khartoum, Sudan kuch...

Kuchelewa uwanjani kwamponza Sadio Mane

Picha
Meneja wa Southampton Ronald Koeman ametoboa siri kuwa jana alilazimika kumwondoa Sadio Mane ambaye ni raia wa Senegal kwenye orodha ya wachezaji watakaonza katika mechi dhidi ya Liverpool kwa kosa la mchezaji huyo kuchelewa kuingia uwanjani. Koeman amesema ilibidi kumweka mchezaji huyo pembeni na kumpanga mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Benifica Philip Jurisichi kuchukua nafasi yake. Koeman alisisitiza kuwa timu hiyo imejiwekea kanuni ambazo ni lazima kila mtu azifuate . Katika mechi hiyo Southampton wakiwa nyumbani walipata kichapo cha magoli mawili kwa bila majibu kutoka kwa Liverpool katika mechi ya lidi kuu ya England. Hata hivyo Koeman amejitetea kwamba pamoja na kipigo hicho cha jana bado ana matumaini kuwa timu yake itamaliza msimu wa ligi hiyo ikiwa katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi. Sadio Mane anayechezea Southampton

Al-Sisi,aomba msaada dhidi ya IS

Picha
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema kuna haja majeshi ya muungano wa jumuiya ya kiarabu ya Pan-Arab kutoa majeshi yao ili kukabiliana na ugaidi. Amesema kuwa mataifa kadhaa yametoa majeshi yao kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Kiislam wa Islamic State tangu kuuawa kwa Wakristuhuko nchini Libya. Mataifa yaliyotoa misaada ya kifedha na kijeshi ni Jordan,Falme za Kiarabu na Marekani kwa lengo la kuangamiza kundi hilo Syria na Iraq. Akizungumza kupitia Televishen Sisi amesisitiza misaada ya kifedha kutoka mataifa ya Saud Arabia ambao walisaidia wakati wa kuuangusha utawala wa aliyekuwa Rais wa Kiislam wa Mohammed Morsi. Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

Mia tano waokolewa machimboni Afrika Kusini

Picha
Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini. Moto mkubwa uliripuka mapema mwanzoni mwa wiki hii umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg. Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo . Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea. Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo. Mchimbaji akiokolewa na wafanyakazi wa kitengo cha zimamoto

Kenya na TZ kutatua mgogoro wa kitalii

Picha
Maafisa wa serikali kutoka Tanzania na Kenya watakutana mjini Arusha mwezi ujao ili kutafuta suluhu ya kutatua mzozo kuhusu marufuku ya magari ya kitalii kutoka Tanzania kuingia katika uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tangu Disemba mwaka uliopita. Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Katibu wa kudumu katika wizara ya madini, mali asili na utalii Daktari Adelhelm Meru amesema kuwa swala hilo ni la kibiashara na halikuweza kuwasilishwa mbele ya kikao cha marais wa Afrika mashariki kilichokamilika jijini Nairobi. Amesema kuwa mkutano huo utafanyika mjini Arusha mwezi Machi tarehe 18 hadi 20 na anatarajia kupata suluhu ya muda mrefu ya mgogoro huo,ambao huenda ukaathiri uhusiano kati ya mataifa haya mawii ambayo yanashindania Utalii katika eneo hili. Tangu mwezi Disemba mwaka uliopita,mamlaka ya Kenya iliweka marufuku ya magari yote ya kitalii kutoka Tanzania kutoingia katika uwanja wa Ndege wa Jomo kenyatta Jijini Nairobi ikidai kwamba inaidhinisha makubaliano ya...