Mia tano waokolewa machimboni Afrika Kusini
Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini.
Moto mkubwa uliripuka mapema mwanzoni mwa wiki hii umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo .
Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea.
Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo.
Mchimbaji akiokolewa na wafanyakazi wa kitengo cha zimamoto |
Maoni
Chapisha Maoni