Kuakhirisha uchaguzi kwapunja demokrasi

Chama kikuu cha upinzani cha Nigeria kimesema kuwa kuakhirishwa kwa uchaguzi mkuu kumerejesha nyuma demokrasi.
Mkuu wa tume ya uchaguzi, Attahiru Jega, alisema upigaji kura hauwezi kufanyika Jumamosi ijayo kwa sababu wanajeshi wanaotakiwa kulinda vituo vya kupigia kura wanatumika kupigana na Boko Haram:
"Hatari ya kutumia vijana wetu katika jeshi na kuwataka watu watumie haki yao ya kidemokrasi, katika hali ambapo hawawezi kuhakikishiwa usalama wao, ndio jukumu letu kubwa.
Katika hali hiyo tunaamini kuwa mashirika machache ya uchaguzi popote pale duniani yatafikiria kusonga mbele na uchaguzi kama ilivyopangwa, katika hali kama hii."
Bwana Jega alikanusha kuwa alishinikizwa aakhirishe uchaguzi; lakini siku ya Alkhamisi tu alikuwa akisisitiza kuwa uchaguzi utafanywa kama ulivyopangwa.
Chama cha upinzani cha APC kimesema jeshi limetaka uchaguzi uakhirishwe ili kusaidia kampeni ya Rais Goodluck Jonathan.
Waandishi wa habari wanasema haikuelekea kuwa usalama ndani ya nchi utatengenea sana katika wiki sita tu zijazo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji