MV Dar es Salaam yaanza majaribio, yaenda bagamoyo na kurudi Dar
Waziri wa Ujenzi Dk, John Magufuli leo amewaongoza wananchi wa jiji la Dar es Salaam kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari zake kati ya Dsm na Bagamoyo.
Mamia ya wananchi wakiwa na furaha ya usafiri huo wamesafiri pamoja na Waziri Dk Magufuli bure kutoka jijini Dar hadi Bagamoyo kwenda na kurudi kujionea huduma hiyo itakayoanza kutolewa siku za usoni.
Akizungumza kwenye majaribio hayo Waziri Dk Magufuli amesema lengo la Serikali kufanya hivyo ni kutaka kuharakisha maendeleo ya wananchi kwa njia yeyote akiongeza kuwa usafiri wenye tija unaongeza pato la taifa.
Amesema Kivuko hicho kitazinduliwa rasmi hivi karibuni na kuanza safari zake mara moja, hivyo wasafiri wanaokwenda bagamoyo hawatalazimika tena kutumia barabara.
"Mbali na kuongeza pato la taifa pia kivuko hiki kitapunguza kwa namna moja ama nyingine foleni za jiji la Dar es Salaam, amsema Magufuli.
Maoni
Chapisha Maoni