Bei ya Mafuta yashuka zaidi Tanzania
Mamlaka ya udhibiti wa Nishati ,Maji na mafuta EWURA nchini Tanzania imetangaza punguzo la jingine la mafuta nchini humo hali inayoleta matumaini tofauti,huku baadhi ya wananchi wakitaraji kunufaika kwa kupungua kwa gharama nyingine za huduma ya usafiri,lakini bado wamiliki wa mabasi ya masafa marefu wanasema punguzo hilo halina unafuu wowote kwao.
Afisa mahusiano wa EWURA nchini Tanzania Titus Kaguo amesema kuwa pamoja na punguzo hilo lakini ingeweza kupungua hadi kufikia chini ya dola moja yaani shilini 600 za kitanzania,lakini kiwango hicho hakijafikiwa kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.
Akizungumzia utekelezaji wa amri ya mamlaka hiyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kushusha bei,Kaguo amesema kuwa kwa sasa wanakusanya taarifa kutoka nchi nzima ili kubaini wanaokaidi amri hiyo.
Kwa upande wao wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani baadhi yao,wamesema kuwa punguzo hilo halina manufaa kwao kuwawezesha kushusha gharama za usafiri kwa kuwa gharama zingine za uendeshaji hazijapungua.
Yudika Mremi ni mmiliki wa kamupini ya mabasi ya Dar Express yaendayo mikoani,anasema kuwa gharama za uagizaji wa mabasi na vipuri bado kodi yake ipo juu.
hatua ya kushuka kwa bei ya mafuta huenda watu wakapata nafuu ya gharama za maisha |
Maoni
Chapisha Maoni