Baba amuunguza vibaya mdomo Mtoto wake miaka saba kwa kosa la kudoko maharage

Baba amuunguza vibaya mdomo Mtoto wake miaka saba kwa kosa la kudoko maharage

Mwemezi Muhingo Kibondo

Vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa Wanawake na watoto vinaendelea kushika kasi  licha ya Serikali na mashirika mbalimbali ya haki za Binadamu  kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu  visijiokeze tena

Haliyo hiyo imejitokeza tena katika kijiji cha Kasaka Kata ya Nyaruyoba Wilaya ya Kibondo  mkoani kigoma baada ya Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Sindotuma Nyamubi,  kumchoma moto na kumuunguza vibaya sehemu za mdomoni  wake, mtoto wake wa miaka saba akimtuhumu kudokoa maharage yaliyotakiwa kutumika kama mboga kwa ajili ya kulia chakula

Afisa  mtendaji wa kijiji hicho Bwa Felix Cosmas amesema kuwa mtoto huyo alibainika kuwa amefanyiwa kitendo hicho baada ya majirani kutomuoana akicheza na wenzake kwa muda wa siku tatu kama  ilivyokuwa imezoeleka, ndipo walipogundua alikuwa amefichwa ndani  ya nyumba na kugundua tatizo hilo na kutoa taarifa  hatua iliyofanikisha mzazi huyo kukamatwa na kufikishwa Polisi


 Nae Afisa Usitawi wa jamii wilaya ya Bi Sofia Gwamagobe amesema kuwa  ni vizuri wazazi na walezi kutambua na kujali hali za watoto na pia jamii inatakiwa kuendelea kufichua na kutoa taarifa katika vyombo husika  ili kuweza kuokoa maisha watu wanaofanyiwa mambo kama  hayo kama wamejeruhika kuwapatia matibabu kabla hawajapata madhara makubwa


Hata hivyo mkuu wa jeshi la polisi wilayani hapo,  amekili kuwepo kwa tukio hilo, na kumtaja aliyejeruhiwa vibaya kuwa ni Shukuru Sindotuma  na amesema baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa kituoni hapo, amekubali kuwa alimchoma moto mtoto wake   kwa kosa la kula maharage bila ruhusa yake


Aidha Joshua amesema  kuwa  Mthumiwa huyo atafikishwa mahakani muda wowote ili taratibu za kisheria zifuate, pia amewataka  wazazi na walezi kuacha Tabia ya kuwaadhibu watoto wao kuwa kuwapa adhabu kubwa kupita kiasi kwa mambo matendo usababisha madahara makubwa kwa wahanga katika kufiri na hali za kawaida za maisha yao  


Nao baadhi wazazi wakazi wa kibondo wamelaani kitendo hicho kilichofanywa na mzazi mwenzao kuwa ni kitendo cha kikatili na kuwataka wanajamii kuacha kutumia hasira kali kwa watoto wadogo

Mtoto huyo Shukuru Sindotuma alikuwa anaishi na baba yake na mdogo wake mmoja wazazi wao wakiwa wameengana na   amelazwa katika Hopitali ya wilaya ya kibondo akitibiwa majeraha yake
Mwisho


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao