Wapiganaji 300 wa Boko Haram wauawa
Jeshi la Nigeria limesema kuwa
limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi
hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini
mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Maoni
Chapisha Maoni