Watanzania isomeni Katiba pendekezwa ndipo muwe na maamuzi ya kuipigia kura ya ndiyo, au hapana


Watanzania wametakiwa kuwa na tabia ya kujisomea mambo mbalimbali ili waweze kuwa na uelewa katika kila jambo wanalo lifanya na kuwa na maamuzi yenye tija

Kauli hiyo, imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wa wilaya ya kibondo 
Emmanuel Gwegenyeza aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya kiziguzigu wilayani Kakonko mkoa wa kigoma,kwakuandaliwa na chama hicho kwa ajili ya kuielimisha jamii  kuhusu swala la maamuzi ya kuipigia kura katiba inayopendekezwa April 30 mwaka huu.

Gwegenyeza amesema kuwa jamii kwa ujumla imekuwa ikiyumbishwa na baadhi ya makundi ya watu, na wanasiasa, kuikataa katiba   hali watu wengi hawaijui na wala  hawafahamu hata maana ya katiba nini, ili watu waweze kufahamu ni vema kila mtu aisome atakapoelewa maana yake na kujua kilichomo apige kuara ya kuikataa au kuikubali

       
Aidha amewataka viongozi wa  vyama vya siasa makundi mbalimbali, na serikali kuhakikisha wanatoa elimu na ushawishi kwenye jamii kwakuwa swala hili siyo la majaribio bali kila mtu anatakiwa kuwa makini kwasababu huo ni mkataba



 Baadhi ya wananchi wamekataa mawazo ya baadhi ya viongozi wanaojitaidi kuwashawishi wananchi kupiga mkura ya ndiyo juu ya katiba bila kujua kilichomo ni kuwanyima haki na siyo uzalendo bali ni vema kila mtu anatakiwa  aweze kupewa uelewa hususa watu wanaoishi vijijini


Pamoja na mambo mengine baadhi ya  wananchi ambao ni Sakina Abdalah na Daudi Jonas, wamema kwenye mkutano huo kuwa wanakabiliwa na matatizo mengi katika maisha yao ya kila siku ikiwa Afya  na ukosefu wa maji safi na salama katika vijiji vya kata hiyo, hali inayokwamisha shuguli za maendeleo na uzalishaji mali kwa kutumia muda mrefu wakitafuta maji hasa kwa upande wa vijijini


Julias Mbwiga ambaye ni katibu wa cama cha Mapinzi Wilaya ya kakonko akisoma lisara  katika mkutano huo amesema kuwa kufikia mwaka 1977 wilaya ya kakonko hakuwa na visima vyaji safi na salama lakini hivi sasa vipo visima 50 na visima virefu 34 lakini kati ya hivo ni vichache vainavyofanya kazi na kuiomba serikali iongeze nguvu katika kuboresha miundo mbinu ya maji


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw, Lenatus Damian amesema kuwa zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikisababisha kukosekana kwa maji hasa vijijini ikiwa ni kilimo cha uvamizi katika vyanzo vya maji kinachosababisha uharibifu wa mazingira na pia na kutokuwepo na uimarishaji wa mifuko ya watumia maji hasa vijijini na miundo mbinu inayokuwa imeengenezwa inapoharibika ukarabati unashindikana kwa sababu ya ukosefu wa fedha


Hata hivyo amesema zipo juhudi zinazofanyika kupitia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na vyombo vya watumiaji maji kwa kujenga miundo mbinu na kukarabati iliyopo kuhakikisha maji yanapatika na kuondoa usumbufu kwa wananchi katika kijiji cha kiziguzigu ambacho ndicho chenye shida kubwa ya maji
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao