Kiev imeanza zoezi la kuondoa silaha nzito
Vikosi vya Ukraine vimeanza Ijumaa wiki hii zoezi la kuondoa silaha nzito mashariki mwa Ukraine, ambapo makubaliano ya kusitisha vita yameonekana kuheshimishwa kwa Hatua hii ya mwanzo itachukua masaa 24 na itafuatiwa na uondoaji wa vifaa vya kurusha roketi na vifaa vingine vizito, amebaini msemaji mmoja wa jeshi alipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.
.
Iwapo zoezi hili litathibitishwa, itakua ni hatua ya kwanza ya uondoaji wa silaha nzito, zoezi ambalo liitaangaliwa kwa makini na jumuia ya Usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE).
Kulingana na makubaliano ya Minsk 2 yaliyotiliwa saini Februari 12, zoezi la kuondoa silaha nzito lingelipaswa kuanza Jumapili iliyopita, lakini serikali ya Ukraine iliomba kwanza uheshimishwaji wa jumla wa usitishwaji wa mapigano kwa upande wa waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki. Lakini usitishwaji wa mapigano umetekelezwa kwenye uwanja wa vita.
Hata hivyo, vikosi vya Kiev vimelani mwenendo wa waasi ya kuongeza idadi ya wapiganaji karibu na mji wa Marioupol, wakiwemo wanajeshi wa Urusi. Mji huo wa Marioupol umekua ukitazamiwa kulengwa hivi karibuni na waasi..
Maoni
Chapisha Maoni