Cannavaro aomba Watanzania kuiombea Yanga

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” amewaomba Watanzania kuiombea timu yake ili ishinde mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao, BDF XI ya Botswana.
Yanga watasafiri wikii hii kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi kwanza. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam takriban wiki moja iliyopita, Yanga, ikiwa chini ya kocha Mdachi, Hans Pluijm, walishinda 2-0.
“Watanzania watuombee ili tushinde na kusonga hatua ya pili”, alisema Cannavaro, baada ya Yanga kuwafunga Mbeya City 3-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara na kuongoza ligi wakiwa na pointi 31.
“Mechi ya ugenini (away) mara nyingi huwa ni ngumu, tulishinda Dar es Salaam na tunahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili tusonge, Watanzania watuombee sisi na wenzetu Azam kwa sababu tunawakilisha nchi”, alisema Cannavaro.
Yanga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC watakuwa na vibarua vya ugenini mwishoni mwa wiki.
Azam watasafiri kwenda Khartoum, Sudan kucheza na El-Merreikh katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Azam ikiwa chini ya kocha Mcameroon, Joseph Omog walishinda 2-0.
Cannavaro akiwa kazini

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji