Jeshi la Ukraine kuondoka mji wa vita
Rais wa Ukraine Petro Poroschenko
amesema kuwa majeshi ya Ukraine yanakaribia kumaliza mipango yake ya
kuondoka mji wa Debaltseve kuliko na mapigano.
Picha za runinga zinaonyesha milolongo ya vifaru na magari mengine ya kijeshi pamoja na wanajeshi wakiondoka maeneo hayo.
Bado milio ya risasi na mizinga inasikika licha ya kutiwa saini kwa muafaka wa kukomesha vita na kuondoa silaha nzito nzito toka mji huo kutiwa saini juma lililopita.
Sasa anaelekea mashariki mwa taifa ili kuwalaki wanajeshi wake.
Maoni
Chapisha Maoni