Wakristo 21 wa madhehebu ya Coptic, raia wa Mirsi, wamekatwa vichwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu nchini Libya, lenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Picha za waumini hao ziliyorushwa kwenye mtandao zimezua hisia kali nchini Misri na ulimwengu wa Kiarabu. Kanisa la Kicoptic na Msikiti mkuu wa al-Azhar vimelani uhalifu huo wa kigaidi, wakati rais wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi, akitangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Cairo, Alexandre Buccianti, picha ziliyorushwa kwenye mtandao zilionyesha waumini hao wa madhehebu ya Coptic wakivaa nguo za rangi ya machungwa wakikusanywa sehemu moja na watu waliokua wakivalia nguo nyeusi wakificha nyuso zao, huku wakiwalazimisha kupiga magoti karibu na bahari.
Katika video hiyo Wakristo hao wameonekana wakitikisa midomo yao, ikiaminika kuwa wamekua wakifanya maombi ya mwisho, kabla ya kuchinjwa. Msemaji mmoja amesema kuwa kitendo hicho ilikua ulipizaji kisasi kwa Osama Bin Laden, ambaye inasadikiwa kuwa aliuawa na kutupwa baharini.

Hali hiyo inatokea wakati kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu nchini Libya lilitangaza siku tatu ziliyopita kwamba liliwauawa waumini hao wa madhehebu ya Coptic, tangazo ambalo limethibitishwa na picha ziliyorushwa kwenye mtandao, ambazo televisheni ya Misri ilikataa kuzirusha hewani.

Familia za wahanga kutoka mkoa wa Minieh ambapo kuna idadi kubwa ya Wakristo wa madhehebu ya Coptic, walijielekeza siku tatu zilizopita katika mji mkuu wa Misri, Cairo, kuoimba serikali ya Misri kuingilia kati ili kuwaokoa ndugu zao. Familia hizo ziliandamana katika Kanisa la Wakristo wa madhehebu ya Copitc, kisha mbele ya Ofisi ya chama cha wanahabari kabla ya kupokelewa na Waziri mkuu, ambae aliahidi kwamba serikali itafanya kiliyo chini ya uwezo wake ili kuwaokoa waumini hao. Lakini muda ulikua ulishapita.

Hata hivyo rais wa Misri amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kwa namna yoyote ile inayoona inafaa katika kulipiza kisasi cha mauaji ya kundi la Wakristo wa madhehebu ya Coptic yaliyofanywa na kundi la wapiganaji wa jihad nchini Libya lenye mafungamano na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji