Kenya na TZ kutatua mgogoro wa kitalii

Maafisa wa serikali kutoka Tanzania na Kenya watakutana mjini Arusha mwezi ujao ili kutafuta suluhu ya kutatua mzozo kuhusu marufuku ya magari ya kitalii kutoka Tanzania kuingia katika uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tangu Disemba mwaka uliopita.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Katibu wa kudumu katika wizara ya madini, mali asili na utalii Daktari Adelhelm Meru amesema kuwa swala hilo ni la kibiashara na halikuweza kuwasilishwa mbele ya kikao cha marais wa Afrika mashariki kilichokamilika jijini Nairobi.Amesema kuwa mkutano huo utafanyika mjini Arusha mwezi Machi tarehe 18 hadi 20 na anatarajia kupata suluhu ya muda mrefu ya mgogoro huo,ambao huenda ukaathiri uhusiano kati ya mataifa haya mawii ambayo yanashindania Utalii katika eneo hili.
Tangu mwezi Disemba mwaka uliopita,mamlaka ya Kenya iliweka marufuku ya magari yote ya kitalii kutoka Tanzania kutoingia katika uwanja wa Ndege wa Jomo kenyatta Jijini Nairobi ikidai kwamba inaidhinisha makubaliano ya mwaka 1985 na Tanzania kuhusu ushirikiano wa Utalii.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao