kumi na wawili waalikwa Tanzania:magongo

Wachezaji 12 wa kriketi kutoka nchi za Pakistan, India, Afrika ya Kusini na Uingereza wawasili nchini Tanzania mwezi ujao kushiriki katika michuano maarufu ya APL T20 (kwa wanaume) inayoshirikisha wachezaji wenye kiwango cha juu.
Michuano hiyo, kwa mujibu wa Afisa wa Chama Cha Kriketi Tanzania (TCA), Kazim Nasser, inaanza Machi 12 na itadumu kwa muda wa juma moja. Kila nchi itapeleka Tanzania wachezaji watatu wa kiwango cha juu watakaopendekezwa na vilabu/vyama vyao baada ya mwaliko.
Kutakuwa na timu nne na kila timu itajumuisha wachezaji watatu. Wachezaji wazawa watatoka katika timu ya taifa ya wakubwa na wengine kadha wanaochipukia.
Kwa mujibu wa Nasser, lengo la kualika wachezaji wanaocheza kriketi ya kulipwa (professional) ni kuwapa uzoefu wachezaji wa Tanzania na kubadilisha uzoefu.
Michuano hiyo inakuja baada ya Tanzania kuandaa michuano ya vijana chini ya miaka 19 ya Afrika siku tatu zilizopita kwa ajili ya kufuzu kucheza kombe la Dunia ambapo Namibia waliibuka mabingwa na kufuzu.
Michuano ya APL ilianzishwa mwaka 2009 na TCA imekuwa ikialika wachezaji kutoka nchi za Afrika, Ulaya na Asia.
Katika michuano ya mwaka jana, TCA pia ilialika wachezaji kutoka katika nchi hizo nne.
Katika michuano ya miaka ya nyuma, wachezaji maarufu kutoka Kenya waliowahi kucheza kombe la Dunia zaidi ya mara tatu, Jimmy Kamande na Steve Tikolo ni miongoni mwa waliowahi kushiriki.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji