Vikosi vya Chad vyawaua wapiganaji 200
Jeshi la Chad linasema kuwa limewaua wapiganaji 200 wa kundi la boko Haram huku nao wakipoteza wanajeshi 9 katika vita vikali vya kuuteka mji muhimu kazkazni mashariki mwa Nigeria.
Wapiganaji wa Boko Haram waliwauwa watu 30 baada ya kutoroka mapigano hayo na kuelekea nchini Cameroon,mkaazi mmoja amesema.
Vilikuwa vita vikali vilivyowahusisha wapiganaji wa Chad tangu waingie Nigeria ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Vikosi vya Chad na vile vya Cameroon pia vinaendelea kuangusha mabomu katika msitu mkubwa wa sambiza ambapo wapiganaji hao wana kambi.
Boko Haram wanadaiwa kutorokea katika katika msitu huo baada ya kuwateka zaidi ya wasichana 200 wa shule mnamo mwezi Aprili kutoka mji wa kazkazini mashariki mwa Nigeria wa Chibok.
Haijulikani iwapo bado washichana hao wapo katika msitu huo.
Maoni
Chapisha Maoni