Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2015

Akutwa hai kwenye kifusi, Nepal

Picha
Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano zilizopita. Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi. Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo. Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu. Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 k

Askari wa Ufaransa wanajisi watoto CAR

Picha
Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wanachunguza tuhuma za ngono kwa watoto zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa nchi hiyo pindi walipokuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wizara ya Ulinzi imesema itahitaji kutolewa kwa adhabu kali zaidi dhidi ya yeyote atakae patikana na hatia. Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kupatikana kwa nyaraka zilizotolewa mwezi July na mfanyakazi mwandamizi wa Umoja wa Mataifa. Afisa huyo alisimamishwa kazi baada ya kupewa nyaraka hizo za siri kwa Ufaransa. Farhan Haq, msemaji msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, amesema Umoja wa Mataifa umefanya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambazo itazifuatilia kwa kina. Mmoja wa wanajeshi wa Ufaransa

Escrow yampa tuzo Kafulila

Picha
Dar es Salaam.  Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow limemng’arisha Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi),  David Kafulila baada ya kutunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kufichua ufisadi huo uliohusisha uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Katika sakata hilo, mawaziri wawili walipoteza nyadhifa zao pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuwahusisha na sakata hilo. Maofisa wengine kadhaa wa Serikali wamesimashwa au kufunguliwa mashtaka kutokana na kuhusika kwao kwenye ufisadi huo. Sakata hilo lililoteka kwa kiasi kikubwa mkutano wa Bunge wa 16 na 17 kabla ya kufika bungeni,  liliibuliwa na Gazeti la The Citizen, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd na Kafulila kuwasilisha hoja ndani ya Bunge ili kujadiliwa. Tuzo aliyopewa Kafulila jana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadam

Korea Kaskazini yaua maafisa serikalini

Picha
Shirika la kiinteligensia la Korea kusini linasema utawala wa Korea kaskazini ,mwaka huu, umewauwa watu waliokuwa na nyadhfa za juu wapatao 15 , wanaodhaniwa kuwa wapinzani wa utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un, kama njia ya kunyamazisha upinzani nchi humo. Mmoja wa wanaripotiwa kuuawa alikuwa naibu waziri aliyelalamikia na kukosoa sera ya misitu nchini humo. Habari hizi zilitokea wakati shirika hilo la kiintelijensia lilipozungumza na kundi la watunga sheria wa huko Korea Kusini. Korea kazkazini haijatoa kauli yoyote kuhusiana na madai hayo lakini uongozi wa nchi hiyo umewahi kuwauwa baadhi ya wapinzani wao. Rasi wa korea Kaskazini Kim Jong Un

Ulanguzi wa watu ni mkubwa Libya

Picha
Uchunguzi wa BBC nchini Libya umebainisha mtandao mpana unaotumiwa na walanguzi wanaopata mamillioni ya dolla kupitia usafirishaji wa watu kinyume cha sheria. Mtu mmoja anaehusika na biashara hiyo amesema kuwa wingi wa watu waliotaka kusafirishwa kwa njia hizo za panya na za hatari umewafanya kuongeza malipo wanayowatoza wahamiaji hao kwa 400%. Mtu huyo amekiri kuwa boti ndogo wanazotumia ni hafifu lakini hujazwa watu ambao tayari wamewalipa si chini ya dolla 450 kila mmoja, kwa safari hiyo ya kubahatisha ambayo ni dhahiri wengi wao huenda wakapoteza maisha yao. Mwandishi wetu wa BBC aliyefanya uchunguzi huo anakadiria biashara hiyo kuwa ya thamani ya dolla millioni mia moja na hamsini kila mwaka. Hivyo ni dhahiri kuwa kundi la wahalifu hao linajitajirisha, na kuwasabishia wengi maafa ya kufa maji na mengineyo , lakini kwa sababu ya ghasia , vita na kuporomoka kwa utawala wa Libya hamna yeyote anaewadhibiti wala kuwawajibisha wahalifu hao. Wahamiaji wakiokolewa baharini

69 wahukumiwa maisha Misri

Picha
Mahakama ya Misri imewahukumia kifungo ncha maisha jela, watu 69 baada ya kupatikana na hatia kuchoma kanisa moja nchini humo. Kanisa hilo liliteketezwa moto wakati machafuko yalipozuka eneo la Kerdasa karibu na mji wa Cairo mwaka 2013. Makabiliano makali yalizuka pale jeshi lilipoanza kuwaondoa wafuasi wa aliyekua Rais Mohammed Morsi kutoka maeneo waliokua wakiandamana. Mamia ya waandamanaji waliuawa kwenye operesheni hiyo. Mahakama nchini Misri

Nepal yasema inasimamia vyema misaada

Picha
Serikali ya Nepal imejitetea dhidi ya lalama kwamba inashindwa kusimamia vyema misaada ya dharura, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi hapo Jumamosi. Mkuu wa masuala ya dharura wa Nepal Rameshwor Dangal,ameambia BBC serikali inajitahidi iwezavyo, lakini mkasa huo ulikumba majimbo 20 nchini, na hivyo mahitaji ni mengi sana ndiposa serikali inalemewa. Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji mkuu wa taifa hilo. Maelfu wameanza kuuhama mji huo mkuu. Wanajeshi wakitoa misaada Nepal

Maandamano:Jeshi lasambazwa Burundi

Picha
Jeshi la Burundi limetawanywa nchini humo kujaribu kukabiliana na wale wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu. Polisi walivunja maandamano ya Wanaharakati na wapinzani nchini humo waliongia mitaani kwa siku ya pili kufanya maandamano. Waandamanaji kadha walipigwa risasi jana Jumapili na watu wanne wanaripotiwa kufariki

Warundi 152,572 wawa raia wa Tanzania

Picha
Waliokuwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania zaidi ya 152,572 walioingia nchini humo tangu mwaka 1972, wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania na kuwa huru kuishi kama Watanzania wengine. Wakimbizi hao walikuwa wameomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na waziri wa mambo ya ndani mwaka 2010, sasa ni halali kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za udiwani na ubunge. Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo, mkuu wa makazi ya Mishamo, Frederick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka 2014 katika makazi ya Katumba mkoani Katavi magharibi mwa Tanzania ambako watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye kuhamia katika makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania ambako wakimbizi 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo. Kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Isaack Nantanga amesema hatua ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi hao ni kutokana na hiyari yao na kwamba serikali ya Tanzania ilishauri

Tetemeko laua zaidi ya watu 3,600 Nepal

Picha
Watu wapatao 3,617 wamefahamika kufa katika tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga Nepal Jumamosi. Kituo cha Taifa cha Dharura cha Majanga kimesema watu zaidi ya 6,500 wamejeruhiwa. Watu kadhaa pia wameripotiwa kufa katika nchi jirani za China na India Zaidi ya wapanda milima 200 wameokolewa kuzunguka Mlima Everest, ambao umekumbwa na athari za tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8. Wakaazi wengi wa mji mkuu Kathmandu wamekuwa wakilala katika mahema kwa wale wasio na makazi au wanaohofia kurudi majumbani kutokana na athari zaidi za tetemeko la ardhi zinazoendelea. Maelfu wamelala nje kwa siku ya pili Jumapili, baada ya tetemeko hilo kuipiga Nepal Jumamosi. Maafisa wamesema idadi ya vifo au majeruhi ikaongezeka wakati huu ambapo vikosi vya waokoaji vimefanikiwa kufika katika ameneo ya milimani magharibi mwa Nepal. Taarifa za awali zinasema jamii nyingi za watu, hususan wanaoishi karibu na kingo za mlima, wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na tetemeko hilo. Mtu mmoja amb

Watanzania waliokuwa Afrika Kusini warudishwa

Picha
Dar es Salaam. Serikali imewarejesha nyumbani Watanzania 26 walioathiriwa na mashambulizi yanayofanywa na wazawa dhidi ya wageni katika Jiji la Durban nchini Afrika Kusini. Habari za uhakika zilizopatikana jana Jijini Dar es Salaam, zilieleza kuwa Watanzania hao, walirejea nchini jana alfajiri na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Precision Air. Hata hivyo, jitihada za kumpata Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe hazikuzaa matunda lakini Naibu wake, Mahadhi Juma Maalim alithibitisha habari hizo. “Ni kweli tumewarejesha Watanzania 26 waliwasili leo (jana) asubuhi kutoka Afrika Kusini na hii ilikuwa ni ahadi ya Serikali siku zote tunajali usalama wa raia wetu popote walipo,” alisema Maalim. Hivi karibuni, Waziri Membe alisema kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kuwarudisha Watanzania hao baada ya kutokea machafuko hayo kwa wenyeji kuwapiga na kuwaua wageni kwa kile walichodai ‘kuwaminya’ kwenye ajira

Serikali yataja asasi 24 zitakazofutwa

Picha
Dar es Salaam. Serikali imeanza kutimiza ahadi yake ya kuyafuta mashirika na asasi zisizo za kiserikali, NGO, yakiwamo ya kidini na kwa kuanzia imetangaza kusudio la kuzifuta asasi 24 katika kipindi cha siku saba kuanzia jana. Miongoni mwa asasi hizo ni taasisi mbili za dini ambazo ni Tanzania Muslim Social Community na Tanzania Christian Outreach Ministries ambazo zimepewa siku saba kujitetea. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Issack Nantanga aliliambia gazeti hili kuwa asasi zote zitakazothibitika kwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake, zitafutwa. Nantanga pia alisema panga hilo litazipitia pia asasi ambazo zimekuwa haziwasilishi kwa msajili ada ya kila mwaka na taarifa za fedha zilizokaguliwa na wakaguzi waliosajiliwa. “Haya mashirika 24 ndio tumeanza nayo na ukaguzi unaendelea. Tumetoa muda wa siku saba kuanzia leo (jana) kujitetea kwanini yasifutwe na wakishindwa kufanya hivyo, yatafutwa rasmi,” alisema. Aliyataja mashirika mengine kuwa ni Kagwa Dev

Dk Hoseah awanyatia wagombea urais CCM

Picha
Dar es Salaam. Wakati viongozi wajuu wa CCM wakiendelea kulalamikia makada wanaowatuhumu kutumia fedha kujifagilia njia ya urais, mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah amesema taasisi yake inakusanya taarifa zote za wanachama wa chama hicho tawala wanaotuhumiwa kutumia mlungula. Mara kadhaa viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakiwaonya wanachama wao dhidi ya makada wanaotumia fedha kujitengenezea mazingira mazuri ya kupitishwa na chama hicho kugombea urais, lakini wameeleza kuwa hawawajibiki kuwaripoti Takukuru kwa kuwa ni wajibu wa chombo hicho cha kuzuia na kupambana na rushwa kufanyia kazi malalamiko hayo. Jumatano, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alisema Takukuru hawahitaji kupata mwaliko wa CCM ili kufanya uchunguzi wa kukamata wagombea wanaotumia rushwa ndani ya chama hicho kwani rushwa inayoendelea kwa sasa iko wazi. “Kazi ya kuwafuatilia imeshaanza muda mrefu, tunazo taarifa zao za kutosha kwa kila mwanasiasa anayelalamikiwa,” al

majaribio za chanjo dhidi ya Malaria,

Hatua za mwisho za majaribio za chanjo dhidi ya Malaria, ya kwanza kufikia hatua hii inaleta matumaini kuwa itawalinda mamilioni ya Watoto dhidi ya Malaria. Lakini Majaribio kwa watoto 16,000 kutoka nchi saba za Afrika yameonyesha kuwa kuna mipaka katika matumizi ya dawa hizo na chanjo haifanyi kazi kwa watoto wachanga. Baada ya Watoto kufikia umri wa miezi 5-17 walipewa dozi tatu za chanjo, Kinga ilifanya kazi mwilini kwa kiasi cha 45%. Lakini wataalam wanasema hatua ya kuifikisha chanjo katika hatua hiyo ni kupiga hatua kubwa. Data zilizochapishwa katika jarida moja la maswala ya kitabibu zinaonyesha mafanikio ya chanjo hiyo ni madogo mno kwa vichanga. Wanasayansi wamekuwa wakifanyia kazi chanjo hiyo kwa zaidi ya miaka 20, lakini wachunguzi wa mambo wanaona kuwa bado kazi kubwa inahitajika. RTS,S/AS01 ni Chanjo ya kwanza ya Malaria kufikia hatua za juu za majaribio. kwa sasa hakuna chanjo yoyote dhidi ya Malaria iliyopatiwa kibali duniani. Chanjo hizi zilitolewa ka

Wadukuzi wasoma ujumbe wa Obama

Picha
Gazeti moja nchini Marekani linasema kuwa wadukuzi wa mitandao wa Urusi ambao walifanikiwa kudukua mifumo ya kompyuta ya ikulu ya white house nchini Marekani walifanikiwa kusoma email za rais Obama zisizokuwa za kisiri.. Gazeti la the New York Times linasema kuwa udukuzi huo ulikuwa mkubwa kushinda ule uliothibitishwa na serikali. Wengi wa maafisa wa vyeo vya juu katika ikulu ya Marekani wana kompyuta mbili , moja ikiwa ni ya kisiri na nyingine ambayo inaweza kutumiwa kuwasiliana kote ulimwenguni. Whitehouse

Mateka wa Sweden waachiliwa huru Syria

Picha
Maafisa nchini Sweden wanasema kuwa raia wake wawili ambao walikuwa wakishikiliwa mateka nchini Syria wameachiliwa huru kupitia usaidizi wa utawala wa Palestina na Jordan Watu hao wawili waliripotiwa kutekwa na kundi lenye uhusiano na mtandao wa al Qaeda nchini syria la al-Nusra Front. Waziri wa mambo ya nje nchini Sweden anasema kuwa idara ya ulinzi kwenye utawala wa Palestina, imechukua karibu miezi miwili kusaidia kwenye mazungumzo ya kuachiliwa kwa watu hao. Hata hivyo haijajulikana iwapo fedha ililipwa ili watu hao waachiliwe.

Tetemeko jingine lakumba mji wa Nepal

Picha
Kumeripotiwa tetemeko jingine lenye nguvu nchini Nepal siku moja baada ya tetemeko kubwa lililosabaisha vifo vya karibu watu 2000. Watu walikimbia kwenda maeneo ya wazi kwenye mji mkuu wa Kathmandu wakati kulipotokea tetemeko hilo la vipimo vya 6.7 na kutikisa majengo. Tetemeko hilo nalo lilisikika kaskazini mwa India na Bangaldesh na kusasababisha maporomoko ya theluji katika mlima wa Everest. Ndege za misaada , madaktari na watoa misaada kutoka nchi jirani zimeanza kuwasili nchini Nepal. Ndege kutoka India na China zimetua mjini Kathmandu kusaidia katika jitihada za uokozi. Tetemeko jingine lapiga mji wa Nepal

Watu 2 wauawa katika maandamano Burundi

Picha
Watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi. Waandamanaji wameishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu. Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa. Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo. Ghasia zazuka nchini Burundi

Mayweather:Mimi ni bora kuliko Moh'd Ali

Picha
Floyd Mayweather amesisitiza kuwa yeye ndio bondia bora zaidi kuliko Mohammed Ali. Ijapokuwa amesema kuwa anaheshimu kile kilichochangiwa na Ali katika mchezo wa ndondi,anasema kuwa amefanya zaidi ya Ali kwa kupigana bila kushindwa. Mayweather alisema kuwa yeye ni bora kushinda Mohammed Ali,Sugar Ray kufuatia rekodi yake ya mapigano 47 bila ya kupoteza hata pigano moja. Vilevile ameongezea kuwa hangeweza kushindwa na Leon Spinks aliyemshinda Mohammed Ali mwaka wa 1978.

Maelfu ya watu walala nje Nepal

Picha
Maelfu ya watu nchini Nepal wamelala nje usiku kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo jana Jumamosi ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa na kupotea kwa maisha. Wakazi wa mji wa kathmandu walisema kuwa hawangerudi manyumbani mwao kutokana na hofu ya kutokea kwa mitetemeko zaidi. Serikali ya Nepal inasema inaamini kuwa takriban watu 1500 wameaga dunia lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati makundi ya uokoaji yanapotafuta kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka. Hali mbaya ya hewa inalikumba eneo hilo na watoa huduma za dharura wanasema kuwa huenda ikavuruga jitihada za uokoaji. Watu walala nje Nepal

Kijana aliyewavamia polisi auawa Israel

Picha
Maafisa wa polisi wa Israel Polisi nchini Israeli wanasema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa na kisu kwenye kizuizi kimoja mashariki mwa Jerusalem. Wanasema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 alijaribu kuwadunga kisu maafisa wa mpakani alipokuwa akiwavamia maafisa hao na kisu mkononi. Kisa hicho kilitokea mapema jumamosi karibu na kizuizi cha Al-Zaim Polisi wa Isreali walichapisha mitandaoni picha na kisu ambacho kijana hiyo alikuwa nacho.

Nkurunziza kugombea licha ya pingamizi

Picha
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi June mwaka huu. Usalama umezidi kuimarishwa huku maandamano yakipigwa marufuku kufuatia ombi la upinzani kuwataka watu kuandamana mitaani. Maelfu ya Waburundi wameondoka nchini humo kuhamia nchi jirani kwa hofu ya machafuko kuelekea uchaguzi mkuu. Umoja wa Mataifa umesema Burundi iko katika njia panda ya kura ya haki ama irejee katika kile ilichosema ni hali ya machafuko mabaya zaidi kama ya huko nyuma. Maelfu ya watu walipoteza maisha yao kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2005 nchini humo. Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ameteuliwa na chama chake kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwezi Juni

Tetemeko la ardhi lawaua 1000 Nepal

Picha
Zaidi ya watu mia nane wamepoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal karibu na mji mkuu wa Kathmandu. Polisi wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakishindwa kujulikana walipo kwa hofu huenda wamefukiwa na kifusi. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa saba nukta tisa katika vipimo vya richa limeathiri maeneo ya katikati mwa mji wa Kathmandu na mji wa Pokhara. Majengo kadhaa ya kihistoria yamevunjwa na tetemeko hilo Serikali imetangaza hali ya dharura huku ikisema inahitaji msaada wa kimataifa.    Tetemeko la ardhi mjni Nepal lenye vipimo vya richa 9.7 chanzo  ni Bbc

Droo:Barcelona kuchuana na Bayern Munich

Picha
Klabu ya Barcelona Itakutana na Bayern Munich katika nusu fainali ya kwanza ya kombe hilo. Nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Real madrid dhidi ya Juventus ikiwa ni mkutano wa kwanza kati ya klabu hizo mbili tangu mwaka 2003. Nusu fainali hizo zitachezwa tarehe tano na sita ya mwezi Mei huku mechi ya marudio ikichezwa wiki moja baadaye. katika ligi ya Yuropa,mabingwa watetezi Seville kutoka Uhispania watakabiliana na Fiorentina huku Napoli wakikabiliana na Dnipro kutoka Ukraine. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Mahasimu waombwa kuruhusu misaada S Kusini

Picha
Mashirika ya misaada yanayofanyia kazi nchini Sudan kusini yamezitaka pande zinazohasimiana nchini humo kuruhusu wahudumu wa mashirika hayo kusambaza misaada bila vikwazo. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa wafanyakazi wake watatu hawajulikani walipo baada ya kupota katika jimbo la Upper Nile State mapema mwezi huu . Jana mashirika kadhaa ya misaada yaliondoka katika eneo la Pagak katika jimbo la Upper Nile wakihofia maisha yao .

Togo kumchagua rais mpya jumamosi

Picha
Wapiga kura nchini Togo watamiminika vituoni kesho Jumamosi kumchagua rais mpya kwa muhula mingine wa miaka mitano. Rais wa sasa Faure Gnassingbe, ndiye anatarajiwa kuibuka mshindi katika ya wagombea watano. Amekuwa uongozi tangu mwaka 2005 baada ya kumrithi babake ambaye aliitawala Togo kwa miaka 38. Uchaguzi huo unafanyika licha ya kuwepo malalamiko kutoka kwa upinzani na mashirika ya umma kuhusu kutokuwepo mabadiliko ambayo yatapunguza mihula ya rais. Upinzani ulilalamikia uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010, ukikishutumu chama kinachoongoza kwa wizi wa kura. Rais wa Ghana na mkuu wa Ecowas Dramani Mahama ambaye aliizuru Togo mara mbili zaidi ya siku 30 zilizopita ametaka kuwepo uchaguzi wa amani. Gnassingbe Eyadema, babake rais wa sasa aliaga dunia mwaka 2005 baada ya miaka 38 uongozini, baada ya kuingia madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1967. On Kampeni nchini Togo geza kichwa