Nchi za Ulaya zatakiwa kuokoa wahamiaji

Naibu waziri wa ulinzi nchini Ugiriki amezitaka nchi za kaskazini mwa bara Ulaya kufanya juhudi zaidi kuwaokoa wahamiaji kutoka bahari ya Mediterranean.
Kostas Isichos aliiambia BBC kuwa kile Ulaya ingefanya ni kugawana majukumu ya kukabiliana na janga hilo la kibinadamu.
Amesema kuwa walinzi wa pwani wa Ugiriki wamelemewa na idadi ya wahamiaji na wanahitaji mashua zaidi na helkopta ili kuweza kuokoa maisha.
Pia bwana Isichos amezitaka nchi zingine kuwakubali wahamiaji zaidi. Jeshi la wanamaji la Uingereza linaripotiwa kutathmini msaada ambao litatoa.
Wahamiaji zaidi waliondolewa baharini jana Jumanne na viongozi wa bara Ulaya watazungumzia suala hilo kwenye mkutano ambao utaandaliwa mjini Brussels hii leo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao