Mateka wa Sweden waachiliwa huru Syria
Maafisa nchini Sweden wanasema kuwa raia wake wawili ambao walikuwa wakishikiliwa mateka nchini Syria wameachiliwa huru kupitia usaidizi wa utawala wa Palestina na Jordan
Watu hao wawili waliripotiwa kutekwa na kundi lenye uhusiano na mtandao wa al Qaeda nchini syria la al-Nusra Front.
Waziri wa mambo ya nje nchini Sweden anasema kuwa idara ya ulinzi kwenye utawala wa Palestina, imechukua karibu miezi miwili kusaidia kwenye mazungumzo ya kuachiliwa kwa watu hao.
Hata hivyo haijajulikana iwapo fedha ililipwa ili watu hao waachiliwe.
Maoni
Chapisha Maoni