Watu 2 wauawa katika maandamano Burundi

Watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi.
Waandamanaji wameishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu.Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa.
Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo.
Ghasia zazuka nchini Burundi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Shule ya msingi Nengo ya Walemavu, iliyoko wilayani Kibondo mkoani kigoma, inayohudumia wanafunzi walemavu wa mahitaji maalum inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni ukosefu wa maji Vifaa vya kujinfunza na kufundishia na vyombo vya kulia chakula