Ufaransa yatangaza kumkamata mwanafunzi gaidi

Na RFI
Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja nchini Ufaransa amekamatwa na polisi akiwa na mpango wa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 24 ni raia wa Algeria.

Mwanafunzi huyo anayetuhumiwa kuwa na mpango " kabambe " wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya " kanisa moja au mbili " amekamatwa Jumapili Aprili 20 mwaka 2015 katika mji wa Paris, waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve, ametangaza Jumatano asubuhi wiki.
Mwanafunzi huyo, anaejulikana na Idara ya ujasusi na ambaye alikua " anajiadaa kuelekea Syria " ili kujiunga na katika makundi ya kijihadi, alikuwa na " silaha za kivita aina mbalimbal ".
Mwanafunzi huyo pia anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Aurélie Châtelain, mwanamke mwenye umri wa maiak 32, ambaye alikutwa amefariki katika gari lake siku ya Jumapili Aprili 20 katika kitongoji cha Villejuif karibu na mji wa Paris.
Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve amesema polisi iliendesha msako Jumapili Aprili 20 katika chumba cha kijana huyo baada ya kupata taarifa zake zinazohusiana na kuendesha mashambulizi katika mji wa Paris.
Inaarifiwa kuwa mvulana huyo aliwahi kukamatwa nchini Ufaransa mwaka 2005 kwa makosa mbalimbali.
Hayo yakijri Mahakama kuu ya Indonesia imefutilia mbali rufaa ya Serge Atlaoui dhidi ya adhabu ya kifo aliyohukumiwa na Mahakama nchini humo. Raia huyo wa Ufaransa amepatikana na hatia ya kuingiza mdawa ya kulebya nchi Indonesia. Adhabu hio ya kifo inatazamiwa kutekelezwa wiki ijayo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao