Polis walaumiwa kwa kuwatesa wananchi
Marko Joshua Ocd Kibondo |
Hassan Masala Dc Kibondo |
Herman Vedasto mkazi wa kijiji cha Mulungu akilalamika mbele dc kuhusu mateso wanayopewa na polisi |
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya,Kumhasha kata ya Mulungu na Bunyambo Kata ya Samvula, wamelilalalimkia Jeshi la polisi wilaya ya Kibondo mkoa wa Kigoma kwa kile walichokitaja kuwa ni unyanyasajia dhidi ya Raia wasiyokuwa na hatia
Hayo wamewekwa na wananchi hao, wakimwambia mkuu wa wilaya hiyo, Bw, Hassani Masala mara alipotembea vijiji hivyo kwa ajili ya kujitambulisha kwakuwa mkuu huyo wa wilaya ni mgeni baada ya kuhamishiwa hapo kutoka wilaya ya Kilombero
Herman Vedasto mkazi wa kijiji cha Mulungu na Lazaro Jacob mkazi wa Bunyambo kata ya Samvula walisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya Askali polisi ambao wamekuwa wakiingia kwenye vijiji hivyo, na kuwa kamata wananchi bila sababu na kuwatesa Walimuomba mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anazungumza na jeshi hilo, na kuhakikisha wanadhibitiwa na kuacha tabia ya kuwasumbua wananchi hali
inayoondoa dhana ya utawara bora
Wamesema kuwa waonawaza bora wahamishwe katika kijiji hicho, waletwe watu wengine labda wao hawastaili kuishi katika eneo hilo cha Mulungu japo wanajitambua kuwa Raia halisi wa nchii hii kwa kuwa wanaishi kama wakimbizi bila amani kwenye nchi , alisema Herman Vedastor
Marko Joshua ambaye ni Kamanda wa polisi wilayani humo alipotakiwa kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwa Askali wake alieleza kuwa kila mtu anapaswa kutimiza sheria bila shuruti hakuana polisi ambaye yuko pale kwa ajili ya kusumbua wananchi na nivema wanapoona hali hiyo waeze kutoa taarifa katika ngazi zinazohusika kwa hatua zaidi
Nae mkuu wa wilaya hiyo Hassani Masala ameeleza kuwa, polisi ni chombo kilichopewa dhamana ya kuwalinda laia na mali zao lakini inapotokea Askali anavunja taratibu za kazi, yeye kama mkuu wa wilaya hatavumilia kuona watu wanafanyiwa vitendo visivyostaili na kuwataka wananchi hao kutoa taarifa wanapokuwa wamefaniwa matendo mabaya na askali polisi yeyote ili atakapobainika hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake
Maoni
Chapisha Maoni