Korea Kaskazini yaua maafisa serikalini
Shirika la kiinteligensia la Korea kusini linasema utawala wa Korea kaskazini ,mwaka huu, umewauwa watu waliokuwa na nyadhfa za juu wapatao 15 , wanaodhaniwa kuwa wapinzani wa utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un, kama njia ya kunyamazisha upinzani nchi humo.
Mmoja wa wanaripotiwa kuuawa alikuwa naibu waziri aliyelalamikia na kukosoa sera ya misitu nchini humo.
Habari hizi zilitokea wakati shirika hilo la kiintelijensia lilipozungumza na kundi la watunga sheria wa huko Korea Kusini.
Korea kazkazini haijatoa kauli yoyote kuhusiana na madai hayo lakini uongozi wa nchi hiyo umewahi kuwauwa baadhi ya wapinzani wao.
Rasi wa korea Kaskazini Kim Jong Un |
Maoni
Chapisha Maoni