Tetemeko laua zaidi ya watu 3,600 Nepal

Watu wapatao 3,617 wamefahamika kufa katika tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga Nepal Jumamosi.
Kituo cha Taifa cha Dharura cha Majanga kimesema watu zaidi ya 6,500 wamejeruhiwa.
Watu kadhaa pia wameripotiwa kufa katika nchi jirani za China na India
Zaidi ya wapanda milima 200 wameokolewa kuzunguka Mlima Everest, ambao umekumbwa na athari za tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8.
Wakaazi wengi wa mji mkuu Kathmandu wamekuwa wakilala katika mahema kwa wale wasio na makazi au wanaohofia kurudi majumbani kutokana na athari zaidi za tetemeko la ardhi zinazoendelea. Maelfu wamelala nje kwa siku ya pili Jumapili, baada ya tetemeko hilo kuipiga Nepal Jumamosi.
Maafisa wamesema idadi ya vifo au majeruhi ikaongezeka wakati huu ambapo vikosi vya waokoaji vimefanikiwa kufika katika ameneo ya milimani magharibi mwa Nepal.
Taarifa za awali zinasema jamii nyingi za watu, hususan wanaoishi karibu na kingo za mlima, wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na tetemeko hilo.
Mtu mmoja ambaye aliokolewa na helikopta kwenda katika mji wa Pokhara, kilomita 200 kutoka Kathmandu, amesema karibu kila nyumba katika kijiji chake chenye nyumba zaidi ya 1,000 kimeharibiwa, Bwana Darvas ameiambia BBC
Mmoja wa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Nepal akibebwa na wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao