DC aitaka Idara ya Elimu kutumia fulsa zilizopo katika masomo ya sayansi hata kama serikali haijafikia malengo yake

Idara ya Elimu wilayani kibondo mkoani kigoma,  imetakiwa kuhakikisha inazitumia kwa  manufaa fulsa mbalimbali zinazotolewa na wafadhili katika shule za sekondari ili kufikia malengo yanayokusudiwa hata kama utaratibu wa malengo ya serikali yatakuwa hayajafikiwa.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo bw, Hassani Masala alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata kufuatia agizo la serikali

Hassan Masala Dc Kibondo

Bi Horatha Kabundugulu afisa Elimu sekondari wilaya ya Kibondo
Genifa Kimaro mwalimu shule ya sekonda ya Biturana
Masala ameshangaa baada ya kufika katika shule ya sekondari Biturana na kuona jengo la maabara ambalo limekamil;ika na lina vifaa vyote huku likiwa limefungwa bila kutumika kwa kisingizio cha kukosa walimu wa sayansi hali aliyoitaja kuwa ni uharibifu na kuwanyma haki wanafunzi


Ameongeza kuwa  shule hiyo haina kazi kubwa ya ujenzi  kilichopo ni kuongeza tu vyumba vya kufundishia na walimu wa sayansi  hivyo kinachotakiwa ni kushirikiana na kutimiza matarajio na kujali mali zinazotolewa na wafadhili kwani si watu wengi wanaopaa fulsa kama hizo


Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamedai kwamba wamekuwa wakiambiwa kuwa mwalimu anayehusika na  ufundishaji wa masomo ya sayansi ni mmoja, naye hayupo alipata dharula hivyo kusababisha  wanafunzi kukosa kuitumia bahati hiyo pamoja na kuwepo na vifaa vyote vya kujifunza na kufundishia kama wanavoeleza  Lukas Marko na Sauda  salumu


Bi Honoratha Kabundugulu ni Afisa Elimu shule za sekondari wilaya ya kibondo amemwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa tatizo lililochangia kukwamisha maabara hiyo isitumike  ni tatizo la mawasiliano mabaya kati ya uongozi wa shule hiyo, na Idara ya Elimu hatua iliyolazimisha kufanya mabadiriko ya uongozi huo, huku wanafunzi wengine wakisema kuwa mpango huo wa serikali iwapo kama utakamilika na kuleta mafanikio kwa wanafunzi

Licha hayo walimu nao wamedai kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba za kuishi katika maeneo ya kazi hali inayosababisha walimu kutembea mwendo mrefu  na ufundishaji kuwa hafifu  kwa kutowapatia wanafunzi kile kinachotajiwa kwani wengine wanaishi mbali  na inapofika kipindi cha mvua za masika upata  usumbufu mkubwa


Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kibondo Bw, Fred Elia safu amewaomba walimu wote kuwa wavumilivu kwani wilaya imeshaweka mpango wa kujenga nyumba za walimu tano kila mwaka  kutegemeana na fedha zinazotolewa na serikali na kuwataka kuvuta subira na kufundisha kwa moyo



Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao