Wadukuzi wasoma ujumbe wa Obama
Gazeti moja nchini Marekani linasema kuwa wadukuzi wa mitandao wa Urusi ambao walifanikiwa kudukua mifumo ya kompyuta ya ikulu ya white house nchini Marekani walifanikiwa kusoma email za rais Obama zisizokuwa za kisiri..
Gazeti la the New York Times linasema kuwa udukuzi huo ulikuwa mkubwa kushinda ule uliothibitishwa na serikali.
Wengi wa maafisa wa vyeo vya juu katika ikulu ya Marekani wana kompyuta mbili , moja ikiwa ni ya kisiri na nyingine ambayo inaweza kutumiwa kuwasiliana kote ulimwenguni.
Maoni
Chapisha Maoni