Waendesha Bodaboda 200 Kibondo, wapewa mafunzo ya usalama Barabarani

 Waendesha boda boda Zaidi ya 200 wilayani kibondo mkoani kigoma wanaendelea na mafunzo maalumu ya usalama barabarani yanayotolewa na jeshi la polisi makao makuu kwa kushirikiana na chuo cha future world vocational institute hali itakayosaidia kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na   kutojua sheria za barabarani


Mwenyekiti wa chama cha waendesha boda boda wilayani kibondo  Elisha msigwa jana alipongeza uamuzi wa chuo hicho kuendesha mafunzo hayo kwani yatawasaidia wengi kupata ujuzi na kuzielewa sheria za usalama bara barani ikiwa ni pamoja na kupata lesesni kwa urahisi

Baadhi ya madereva binafsi na madereva boda boda waliopata mafunzo ya udereva wameshukuru kwa kuwa kwanza walikuwa wakiendesha kwa uzoefu bila kujua chochote kuhusu bara bara hivyo mafunzo hayo yatakayodumu kwa sikuk saba yatakuwa chachu ya kupunguza ajali za bara barani zinazosababishwa na uzembe ama kutojua sheria

Askari wa kikosi cha usalama bara barani wilayani kibondo mkoani kigoma Steven  Njoke wp eva alphayo na ally maganga walitoa ujumbe kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto bila kuzijua sheria za usalama barabarani  kuwa inahatarisha usalama wao na Abiria wanaowabeba  na mali  za wa miliki na kusababisha kuwepo kwa walemavu wengi yatima na wajane hali inayopelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa na kudorola kwa maendeleo

Kwa upande wake mkufunzi wa sheria za usalama barabarani kutoka chuo cha future world vocational institute Dar es salaam Patrick Pastory amesema kuwa faida  za mafunzo hayo ni pamoja na kutii sheria bila shuruti, kudhibitiana wao kwa wao wanapokiuka kuvaa kofia ngumu au kubeba mishikaki na hali hiyo inasaidia  kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali 

Mafunzo hayo yanayotolewa bure na chuo cha future world vocational institute cha dare es salaam yataendesha kwa mda wa wiki moja hapa wilayani kibondo kisha yataendelea katika kata mbali mbali za wilaya hiyo ili kuwasaidia madereva kupata cheti cha mafunzo na leseni kwa urahisi

Mkoa wa kigoma una idadi ya ajali za Barabarani zipatazo 5000 kwa kusababishwa na pikipiki hadi mwaka jana ali inayoashiria hatari kubwa na kusababisha madhara makubwa miongoni mwa jamii hatua inayoongezwa na kutokujua au uzembe  wa kufuata sheria za barabarani
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji