Buhari:Tutawarejesha wasichana wa Chibok

Huku Nigeria na ulimwengu kwa jumla ukiadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwanyara kwa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 na wapiganaji wa Boko Haram
rais mteule jenerali mstaafu Muhammadu Buhari amesema kuwa atafanya kila awezalo ili kuwarejesha nyumbani wasichana hao.
Lakini Buhari amekiri kuwa baadhi ya wasichana hao huenda wasipatikane tena.Siku ya Jumatatu,mkaazi mmoja wa mji wa Kazkazini Mashariki wa Gwoza amesema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao
wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka ndani ya nyumba kubwa karibu na kwake.
Maadhimisho ya kutekwa nyara kwa wasichana hao kutoka shule moja ya Chibok yanafanywa kupitia mikusanyiko na maandamano nchini Nigeria pamoja na duniani kwa jumla.
Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za kibinadamu Amnesty International inasema kuwa takriban wanawake 2000 na wasichana wametekwanyara na Boko Haram tangu mwanzo wa mwaka uliopita.Awali rais anayeondoka mamlakani nchini Nigeria Goodluck Jonathan, alisema amesikitishwa kuwa siasa zilipewa kipau mbele,
kuliko maslahi ya wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka shule moja kwenye mjiwa Chibok katika jimbo la Borno.
Rais Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita watapatikana wakiwa salama 
Chanzo ni BBC
Wasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji