Nkurunziza kugombea licha ya pingamizi
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi June mwaka huu.
Usalama umezidi kuimarishwa huku maandamano yakipigwa marufuku kufuatia ombi la upinzani kuwataka watu kuandamana mitaani.
Maelfu ya Waburundi wameondoka nchini humo kuhamia nchi jirani kwa hofu ya machafuko kuelekea uchaguzi mkuu.
Umoja wa Mataifa umesema Burundi iko katika njia panda ya kura ya haki ama irejee katika kile ilichosema ni hali ya machafuko mabaya zaidi kama ya huko nyuma.
Maelfu ya watu walipoteza maisha yao kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2005 nchini humo.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ameteuliwa na chama chake kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwezi Juni |
Maoni
Chapisha Maoni