Mahakama yamuhukumu miaka 45 Gerezani kwa kulawiti
Akuhukumiwa miaka 45 Jera, kwa
kulawiti
Mkazi wa mamlaka ya
mji mdogo wa Kibondo mkoani Kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 45 jela baada
ya kukutwa na hatia katika kosa la
kumkamata kwa nguvu na kumlawiti mtoto
wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Bitare
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya hiyo bw Ismail
Ngaile, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw, Andulile John amemtaja mshitakiwa huyo kuwa ni
Masumbuko Adam, miaka 35 mkazi wa mtaa
wa Maragalasi na kwamba alitenda kosa hilo mnamo march19.2015 katika kijiji cha
Bitare alikokuwa anafanya biashara ya kununua vyuma chakavu
bw Andulile amesema kuwa tarehe hiyohiyo majira ya saa moja
jioni, katika kjiji cha Bitare wakati mtoto huyo alipokuwa ametumwa na Baba
mzazi kumsalimia Bibi yake ndipo mtuhumiwa alimkamata kwa nguvu mvulana huyo na
kumvutia kwenye shamba la migomba na kumtendea kitendo hicho cha kinyama kwa
kumlawiti katika njia ya haja kubwa na mdomoni,
baada ya kuridhika na
ushahidi upande wa mashitaka
uliomba adhabu kali itolewe ukilejea kesi ya nguza Viking kwa jina maarufu babu
seya na wenzake dhidi ya jamuhuri kesi iliyoamuliwa na mahakama ya rufaa ambapo
washitakiwa walihukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya upelelezi kukamilika bila kuacha shaka lolote
mahakama ya hakimu mkazi imezingatia maombi ya upande wa mashitaka na
kumuhukumu mshitakiwa huyo bw Masumbuko Adam kifungo cha miaka 45 jela ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kulawiti ama kuingilia watoto kinyume
na maumbile
Maoni
Chapisha Maoni