Afisa Elimu Afariki gafla akiwa ofisini kwake
Afisa Elimu Afariki gafla akiwa ofisini kwake
Afisa elimu vifaa na takwimu wilayani kibondo mkoani
kigoma bw Jones Biria jana alifariki
ghafla akiwa ofisini kwake alikokuwa akiendelea na shughuli zake za kiofisi
Akizungumza kuhusu historia fupi ya kifo cha marehemu afisa
elimu wa shule za msingi wilayani kibondo Joseph Tirutangwa amesema kuwa kifo
hicho kimetokea jana april 21 majira ya jioni ambapo marehemu alizidiwa ghafla
kisha kupoteza fahamu
Aidha akizungumzia mazingira ya kifo hicho bw Tirutangwa
amesema kuwa marehemu alikuwa anaongea na mlinzi wakiwa wamekaa kwenye viti vya
nje vinavyotumiwa na watu wanaosubiria huduma ndipo marehemu alizidiwa ghafla
kisha haraka akamtuma mlinzi akamuite afisa elimu na alipokuja eneo la tukio
alikuta tayari ameshaanguka na kupoteza fahamu
Bw Tirutangwa amesema kuwa baada ya hari hiyo kujitokeza
marehemu alikimbizwa haraka katika hospitali ya wilaya ya kibondo ambapo kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kibondo dr Kizito Ruhamvya aliyeufanyia
uchunguzi mwili huo, na kuthibitisha
kuwa kifo cha marehemu kimetokana na
shinikizo la damu pamoja na kisukari
Mwili wa Afisa Elimu huyo umesafirishwa kwenda Buseresere
Wilaya ya Chato mkoani Geita kwa ajili ya Mazishi
Maoni
Chapisha Maoni