Mazungumzo ya Iran kurejelewa leo
Mazungumzo juu ya mpango wa nuklia wa Iran yanarejelewa tena mjini Vienna wakati wapatanishi wanapojaribu kupata makubaliano ya mwisho yaliyoafikiwa wiki tatu zilizopita.
Makubaliano hayo yalitajwa kuwa ya kihistoria. Sasa maafisa kutoka mataifa sita yenye nguvu duniani na Iran yanakabiliwa na wakati mgumu wa kujaribu kuchambua masuala ya kina kabla ya mwisho wa mwezi juni.
Iran itahitajika kuacha kurupisha madini ya Uranium ili nayo iwezi kuondolewa vikwazo ambavyo vimeuporomosha uchumi wake.
Maafisa nchini Marekani wanase kuwa waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Johh Kerry huenda akakutana na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif mjini New York siku ya Jumatatu.
Maoni
Chapisha Maoni