Raia wa Yemen wakimbilia Somalia

Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia, 

Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao. Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao. Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao. Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper 
Raia wa Yemen wakivuka katika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo

anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao