Nepal yasema inasimamia vyema misaada
Serikali ya Nepal imejitetea dhidi ya lalama kwamba inashindwa kusimamia vyema misaada ya dharura, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi hapo Jumamosi.
Mkuu wa masuala ya dharura wa Nepal Rameshwor Dangal,ameambia BBC serikali inajitahidi iwezavyo, lakini mkasa huo ulikumba majimbo 20 nchini, na hivyo mahitaji ni mengi sana ndiposa serikali inalemewa.
Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji mkuu wa taifa hilo.
Maelfu wameanza kuuhama mji huo mkuu.
Wanajeshi wakitoa misaada Nepal |
Maoni
Chapisha Maoni