Tetemeko la ardhi lawaua 1000 Nepal
Zaidi ya watu mia nane wamepoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal karibu na mji mkuu wa Kathmandu.
Polisi wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakishindwa kujulikana walipo kwa hofu huenda wamefukiwa na kifusi.Tetemeko hilo lenye ukubwa wa saba nukta tisa katika vipimo vya richa limeathiri maeneo ya katikati mwa mji wa Kathmandu na mji wa Pokhara.
Majengo kadhaa ya kihistoria yamevunjwa na tetemeko hiloSerikali imetangaza hali ya dharura huku ikisema inahitaji msaada wa kimataifa.
Maoni
Chapisha Maoni