Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2014

Watanzania tulieni katika kipindi hiki cha mgawanyiko sababu Escrow

Mwemezi Muhingo Mwanachi Watanzania wametakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki kinachoonekana kuwa  ni cha mapasuko katika Taifa kutokana na upotevu wa pesa ambazo ni mali ya umma toka katika account ya Esrow. Hayo yalisemwa na kiongozi mmjoja wa Dini Mchungaji Eliasi Rugaganya wa Kanisa la kiinjili la Kirutheli Tanzania Dasisi Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Betherehem Nyakato Jijini Mwanza  wakati wa Ibada ya kipaimara iliyofanyika jana Jumapili kanisani hapo. Rugaganya alisema kwakuwa katika nchi yetu ya Tanzania vipo vyombo ambavyo vinadhamana ya kuweza kushugulikia jambo hilo ni vema viachiwe kufanya kazi hiyo na wala wananchi wasijiingize katika migawanyiko inayoweza kusababisha  kuleta shida katia nchi Aidha amevitaka vyombo vyote husika hasa vya kisheria kufanya kazi kwa umakini na uaminifu ili kurudisha Imani ya watanzania waliosambaratika kwa hivi sasa kutokana na kusikia kuwa pesa nyingi kama hizo zinachukuliwa na watu wachache tena...

Bibi harusi wa miaka 14 amuua mumewe kwa sumu kupinga kuolewa

Picha
Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za harusi yake. Kesi hiyo imewashangaza wanaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume anayemzidi umri zaidi ya mara mbili yake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala siyo muhalifu Msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Wasila Tasiu kutoka familia maskini katika eneo lenye idadi kubwa ya Waislamu huenda akakabaliwa na adhabu ya kifo Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama Hamziyya ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi’u pamoja na mumewe Umar Sani wakati bi harusi huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho. Akizungumzia zaidi kuhusu kisa hicho ambacho kimevuta hisia za wengi msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi’u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja...

Bunge la Ufaransa lajadili kuhusu taifa la Palestina

Picha
Moja ya agenda ya kikao cha Bunge la Ufaransa ambalo linakutana Ijuma wi hii hii ni kulitambuwa taifa la Palestina, kabla ya kupigia kura uamzi huo utakaochukuliwa katika kikao hicho. Kura itapigwa Desemba 2 mwaka 2014. Kura hiyo ya ishara haitobadili msimamo rasmi wa Ufaransa. Vikao kama hivyo vya Bunge vimekua vikifanyika katika nchi nyingi barani Ulaya na kupitisha uamzi wa kulitambua taifa la palestina, hali ambayo imekua ikiwapa motisha na faraja raia wa Palestina. Pendekezo la azimio ambalo litajadiliwa na Bunge Ijumaa wiki hii,  “ limeitolea wito kwa serikali ya Ufaransa kulitambua taifa la Palestina” . Wito ambao hauna madhara yoyote kwa msimamo wa Ufaransa, ambayo inabaini kwamba muda haujawadi Palestina kuwa taifa. Ufaransa inaona kwamba mazungumzo kati ya Israel na Palestina ndiyo yatapelekea kuundwa kwa taifa la Palestina. Jitihada za Wabunge na Maseneta wa Ufaransa ni ishara yenye nguvu kwa jumuiya ya kimataifa Qassem Barghouti, mwanae kiongozi wa mamlak...

Hali ya usalama yaendelea kudorora Afghanistan

Picha
Kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan, wametekeleza shambulio la bomu kwenye hoteli moja inayofikiwa na raia wa kigeni, saa chache baada ya mtu mmoja kujitoa muhanga akilenga ubalozi wa Uingereza mjini Kabul. Watu sita wamethibitishwa kufa kwenye mashambulizi haya mawili akiwemo mwanajeshi mmoja wa Uingereza, katika shambulio ambalo ni muendelezo wa mashambulizi yanayofanywa na kundi la Taliban dhidi ya wageni na vikosi vya kimataifa. Vikosi vya usalama nchini Afghanistan vimeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti usalama nchini humo hasa baada ya kupungua kwa askari wa vikosi vya kimataifa ambao baadhi ya nchi zimeanza kuwaondoa wanajeshi wake ikiwemo Uingereza na Marekani. Toka kuanza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakiongoza operesheni za majeshi ya nchi za kujihami za magharibi NATO, wanamgambo wa Taliban wamezidisha mashambulizi wakiwalenga polisi na balozi za mataifa ya magharibi. Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kwa sasa bado...

Mkutano wa kilele wa Francophonie wawekwa chini ya ulinzi mkali Senegal

Picha
Mkutano wa kilele wa Francopfonie unaojumuisha nchi zinazozungumza Kifaransa unaanza Jumamosi Novemba 29 katika kituo cha kimataifa cha mikutano mjini Diamniadio, kwenye umbali wa kilomita 32 na mji mkuu wa Senegal, Dakar. Wajumbe 77, zaidi ya marais na viongozi wa serikali 40, zaidi ya wageni 5000, wakiwemo nusu ya maelfu ya waandushi wa habari wanasubiriwa katika mkutano huo ambao umewekwa chini ya ulinzi mkali. maeneo mbalimbali ya mji wa Diamniadio na maeneo muhimu ya mji mkuu wa Senegal polisi imeimarisha usalama. Kwa mujibu wa chanzo cha usalama, zaidi ya askari polisi 3000 wametumwa katika mji wa Diamniadio. Kikosi cha askari pia kimetumwa katika mji huo, kwani tishio la kigaidi lipo, kama alivyoeleza Jacques Habib Sy, kiongozi wa amati ya maandalizi ya mkutano huo. “Marais, viongozi wa serikali na wageni wajumbe wengine ambao wanashiriki mkutano huo wamelezwa hali hiyo lakini usalama umeimarishwa” , amesema Jacques Habib Sy. Ufaransa imechangia kuimarisha us...

Henry ataka kuisaidia Arsenal

Picha
Uwezekano wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya. Henry huenda akaweka viatu vyake vya soka chini jumamosi wakati ambapo kilabu yake ya New York Red Bulls itajaribu kulipiza kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika fainal ya raundi ya pili dhidi ya New England Revolution. Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amekamilisha kandarasi yake na kilabu hiyo na ijapokuwa anasema kuwa hakuna kilichoafikiwa kuhusu hatma yake ameanza kutoa maoni yake kuhusu maisha yake baada ya kusakata soka. Na baada ya kocha Arsene Wenger kumfungulia milango mchezaji huyo ,Henry amesema kuwa angependelea kuisaidia kilabu yake ya zamani. ''hakuna kilicho wazi''Henry aliliambia gazeti la L'Equipe.''Sijafanya uamuzi wowote na mimi sipendelei uvumi'',. ''Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba nitasalia katika soka kama m...

Wafanyabiashara wa UG waionya Kenya

Picha
Wafanyibiashara wa Uganda chini ya muungano wa Wanabiashara wa mji wa Kampala Uganda KACITA wamelipa Shirika la ukusanyaji Ushuru nchini kenya KRA wiki mbili kuitoa mizingo yote inayoelekea Uganda la sivyo waigomee bandari ya Mombasa. Ilani hiyo iliafikiwa siku ya Alhamisi baada ya saa kadhaa za majadiliano kuhusu athari za hatua ya KRA ya kutoza kodi bidhaa zote zinazoingia katika badari hiyo. Awali ,wafanyibiashara walikuwa wakilipa ada wanayotozwa wakati wanapochukua mizigo yao pamoja na ada nyenginezo. Hatua hiyo kulingana na KACITA si kinyume na matarajio ya jumuiya ya Afrika mashariki pekee bali pia inawaumiza wafanyibiashara wa Uganda pamoja na uchumi. Mwenyekiti wa KACITA Everest kayondo amesema kuwa kufikia jumatano kulikuwa na makasha 4,000 yanayozuiliwa katika Bandari ya Mombasa kutokana na ada za mara kwa mara zinazotolewa na KRA. ''Kwa hivyo tunaipa KRA wiki mbili kutoa mizigo yote ya Uganda la sivyo tuhame hadi katika bandari ya Dar es Salaam'',...

Bunge lasambaratika TZ

Picha
Mzozo mkubwa umesababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku huu wakati likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa Zaidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya nchi hiyo. Taarifa ya mwandishi wa BBC Baruan Muhuza imesema kuwa Bunge hilo, leo limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni saa 4.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Spika wa  Bunge hilo Anne Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali. Hatua hiyo kwa namna Fulani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa...

Mbunge Jimbo la Muhambwe Kizimbani kwa kuzuia uandikishaji wapiga kura

Picha
Mbunge Jimbo la Muhambwe Kizimbani kwa kuzuia uandikishaji wapiga kura Mbunge wa jimbo la Muhambwe mkoani kigoma Bw. Felix Mkosamali amefikishwa katika mahakama ya wilaya ua kibondo mkoani kigoma akikabiliwa na shitaka la kumzuia kalani muandikisha wapiga kura kuto endelea kufanya kazi ya kuandikisha wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa   katika kitongoji cha   Nduta Kijiji cha kumhasha Kata ya Murungu   wilayani kibondo. Mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo, Bw. Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw. Peter Makala amesema tukio hilo limetokea nov.24 alipofika katika kituo hicho nakuzuia wasiendelee kuwaandikisha wananchi na kwamba hali hiyo ni ukiukaji wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.   Bw.makala amesema kitendo cha kuwazuia wananchi hao kujiandikisha kwamba ni kuwanyima haki yao ya msingi ambapo wananchi baada ya kuwazuia waliendelea kudai kujiandikisha   lakini hata hivyo mbunge huyo alizuia kabisa kutoe...

MAAMBUKIZI YA VVU KIGOMA YAPANDA HADI ASILIMIA 3.4

Picha
Takwimu za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa kigoma zinaonyesha kuwa   juu kwa asilimia 3.4 kwa utafiti wa mwaka 2011 na 2012 ikilinganishwa na utafiti wa 2007/2008 ambapo maambukizi yalikua asilimia 1.8 hali ilinayoonekana kusababishwa   muingiliano wa watu toka mikoa mbalimbali hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma Hali hiyo imetajwa kuwa utandawazi pamoja na kuiga mambo ya kisasa miongoni mwa baadhi ya jamii za mkoa huo imekuwa ni chanzo cha ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo na uelewa mdogo Kama ilivyo kawaida   kutokana na mila na destuli za makabila mengi ya Tanzania, jamii na familia nyingi hapa nchini kuna mambo ambayo si lahisi wazazi kuwawekea wazi watoto wao kwa kuhofia uharibifu na kupelekea watoto kufikiri mambo makumbwa zaidi ya umri   hali ambayo inawapelekea kujiingiza katika vitendo vya kufanya mapenzi bila utaratibu na kabla ya wakati Baadhi ya wakazi wa mamlaka ya mj...
r

Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, chanzo ni ikiukwaji wa taratibu kwa viongozi

Picha
Mwemezi Muhingo Kibondo Migogoro ya wakulima na wafugaji  inayoendelea katika maeneo mengi hapa nchini, inasababishwa baadhi ya viongozi kutokuwa elimu juu utambuzi wa migogoro hiyo, na wengine kuacha makusudi kwa kutofuata sheria na taratibu Akitoa taarifa yake kamanda wa polisi wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma SP Marko Joshua. wakati wa semina elekezi kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali na wadau wa maendeleo, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kibondo amesema kuwa jamii kubwa imekuwa ikikosahaki zao za msingi kwa sababu ya baadhi ya viongozi wasiojua na kufuata sheria kwa kuwasababishia migogoro na kugombana wao kwa wao. Joshua aliesema kuwa  wakulima na wafugaji wote wanastaili haki zao kwa mujibu wa sheria za Tanzania na hatua madhubuti hazitachukuliwa kutaingia mgogoro mkubwa ambao itakuwa vigumu kuudhibiti na kusababisha madhara makubwa katika jamii. ‘’Halmashauri nyingi hapa nchini hazijaona kuwa jukumu la kuhakikisha usal...
Picha
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameyashutumu mataifa ya magharibi kwamba yanataka kubadilisha serikali ya Urusi kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine. Aliuambia mkutano wa wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba mataifa ya magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe sera zake kuhusu Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi. Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine. Bwana Lavrov alisema vikwazo hivyo vililenga kuharibu uchumi wa Urusi na kuchochea maandamano.

Lavrov ashutumu mataifa ya magharibi

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameyashutumu mataifa ya magharibi kwamba yanataka kubadilisha serikali ya Urusi kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine. Aliuambia mkutano wa wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba mataifa ya magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe sera zake kuhusu Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi. Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine. Bwana Lavrov alisema vikwazo hivyo vililenga kuharibu uchumi wa Urusi na kuchochea maandamano.

Waliofanya shambulio la Mandera wasakwa

Picha
Maiti za watu waliouliwa na al-Shabaab Jumamosi asubuhi nje ya mji wa Mandera, Kenya, karibu na mpaka wa Somalia, zilipelekwa na wanajeshi hadi mjini humo. Serikali ilikuwa inajitayarisha kusafirisha miili hiyo hadi mji mkuu, Nairobi. Basi lililokuwa limebeba abiria 60 lilitekwa nyara alfajiri na abiria 28 walipigwa risasi na kuuwawa. Wengi waliouwawa ni kutoka maeneo mengine ya Kenya ambao wakifanya kazi Mandera. Inasemekana kuwa wengi wao walikuwa waalimu na wafanyakazi wa wizara ya afya ambao walikuwa wanarudi nyumbani kuwa na familia zao wakati wa Noeli. Msemaji wa wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, alidai kuwa walihusika na shambulio hilo. Wanajeshi na polisi wametumwa huko kwenda kuwasaka wale waliohusika na shambulio hilo lakini hakuna taarifa kuwa wamekamatwa.

Nyalandu: Hatuna mpango kufukuza Wamasai Loliondo

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 eneo la Loliondo mkoani Arusha ni za uongo na uchokozi. Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo. Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu. Akizungumza na waandishi wa habari bungeni jana, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote. “Yaani kwamba sisi tunataka tutume maaskari kuwatoa watu kwenye maboma yao tuyachome moto tuwafukuze? Habari hizo ni za uongo, habari hizo zinataka kuipaka tope nchi yetu na ni za uchochezi na mimi nina uhakika wengi wa mashabiki wa habari hizo ni majirani zetu wa nchi jirani,” alisema. Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao. “Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliond...

Tacaids: Maadhimisho ya Ukimwi kuhakikisha azma ya sifuri tatu inafikiwa

TUME ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), imesema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu imelenga kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti Ukimwi. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids, Dk. Fatma Mrisho, alisema kauli mbiu hiyo pia inalenga kudhibiti Ukimwi Kitaifa na Kimataifa ili kufikia azma ya sifuri tatu. Dk. Fatma alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na Ukimwi, ubaguzi na unyanyapaa inawezekana. Alisema kauli mbiu hiyo inahimiza utekelezaji wa dahati wa malengo ya maendeleo ya millennia na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi. “Azma ya sifuri tatu ni kuhakikisha maambukizi mapya ni sifuri,vifo vitokanavyo na Ukimwi sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2018,”alisema. Pia alisema maadhimisho ya mwaka huu kitaifa yatafanyika mkoani Njombe kuanzia Novemba 24 na kufikia kilele Desemba mosi, mwaka huu....

Mamlaka za vijiji na kata zifuate taratibu

Picha
Viongozi wa serikali za kata na vijiji wametakiwa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kuleta tija na kuondoa minong’ono isiyokuwa na sababu toka wananchi hali ambayo huweza kusababisha kudumaa kwa maendeleo. Hayo yamesemwa na Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya kibondo mkoani kigoma  Bw Dominick Luhamvya wakati warsha ya kujadili miongozo na kanuni za serikali za mitaa ambaye alikuwa alikuwa mwezesha katika warsha ilihiyofanyika  wilayani kibondo. Bw.luhamvya amesema kuwa katika kuweka utaratibu mzuri wa kiuongozi haina budi viongozi kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi wakizingatia haki katika kuwaboreshea miundomnbinu ikiwemo maji,barabara,na shule, ilikuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii kuwa nzuri. Aidha amesema kuwa baada ya watendaji wa kata na vijiji sambamba na madiwani kufanya mikutano na wananchi na mupata kelo mbalimbali kutoka kwa wananchi wataziwasilisha katika balaza la madiwani ambao ndio wenye kikao cha maamuzi. Katika warsha hi...

Kenya kuandaa riadha ya vijana 2017

Picha
Kenya imetangazwa rasmi kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya riadha kwa vijana mwaka 2017, hiyo ni baada ya mji wa Greenboro wa Marekani kujiondoa na kuachia nafasi ya wazi nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye kusifika duniani kwa watimuaji hodari wa mbio. Tangu awali Kenya ilianza kupata unafuu wa ushindani baada ya mji wa Bunos Aires wa Argentina kujitoa mapema. Kenya iliwahi kuandaa mashindano ya dunia ya mbio ndefu za Cross Country mjini Mombasa mwaka 2007. Wakati Kenya ikijiandaa kwa mashindano hayo, Uganda imeshinda ombi la kuandaa mashindano ya dunia ya mbio za Cross Country kwa mwaka 2017 baada ya kuushinda mji wa Manama wa Bahrain. Wakati ambapo mji wa Doha Qatar wenyewe umeshinda kuwa mwenyeji wa mbio za dunia za mwaka 2019.

Raia wa India awekwa Karantini

Picha
India imemuweka karantini mwanaume mmoja ambaye alipatiwa matibabu baada ya kuathirika na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, kwa hofu kuwa huenda akasambaza virusi vya Ebola kwa njia ya kujamiiana. Mtu huyo alipimwa na kukutwa hana virusi vya ugonjwa huo alipowasili Uwanja wa ndege wa Delhi. Hata hivyo Maafisa wamesema amewekwa karantini kwa sababu virusi bado vilikuwepo kwenye mbegu zake za kiume ,ambapo vingeweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana. Vifo vingi vimeripotiwa Liberia,Guinea na Sierra Leone. Wanaume ambao hufanikiwa baada ya matibabu hushauriwa kutoshiriki kitendo cha kujamiiana vinginevyo wahakikishe wanatumia mipira ya kiume,kwa kuwa mbegu za kiume hubeba virusi hivyo kwa siku 90 baada ya kutibiwa. Waziri wa afya wa India amesema mwanaume huyo (26) alifika nchini humo tarehe 10 mwezi Novemba.Amekuwa akibeba nyaraka zake zilizoeleza kuwa alitibiwa maradhi ya Ebola nchini Liberia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya afya, pamoja na ushahidi huo samp...

Bill Gates kusaidia kupambana na Ebola

Picha
Mfuko wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo. Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio. Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi. Mpaka sasa hakuna dawa iliyoidhinishwa wala chanjo ya kupambana na Virusi vya Ebola,matibabu ya hospitalini hutolewa kwa kuwapa wagonjwa maji ili kufunga kuharisha na dawa za kupambana na vijidudu. Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake na namna zinavyofanya kazi. Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF linatarajia kuanzisha majaribio ya tiba Afrika Magharibi mwezi Desemba. Mfuko huo unamilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates na mkewe Melinda umesema kuwa utafanya kazi na washirika kadhaa kwa...

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

Picha
MATUMIZI ya simu kwa wanafunzi shuleni ambayo yamekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwao, yanaweza kudhibitiwa endapo wamiliki wa shule, walimu na wazazi watasimamia sheria zitakazosaidia kuwabana wanafunzi kumiliki simu. Hayo yalibainishwa hivi karibuni wakati wa mahafali ya kwanza kwa darasa la saba na ya saba kwa kidato cha nne katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Mwilamvya Wilaya ya Kasulu mkoani hapa na Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Ziwa Magharibi, Adrian Mlelwa. Mlelwa, alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hutumia simu katika vitendo viovu na kusahau kutekeleza majukumu ya elimu wawapo shuleni. Alisema kuwa kwa sasa ni kipindi cha utandawazi, hivyo mawasiliano ni muhimu kwa kila mmoja, japokuwa katika matumizi hayo kuna madhara na faida zake, na wanaoathiriwa na madhara ya matumizi ya simu ni wanafunzi kwa vile wengi wao hutazama picha za ngono na kutumiana ‘meseji’ za mapenzi wakati wa masomo. “Hatuwezi kuwazuia wanafunzi kutumia simu kuwasiliana na ...

TRA kuwachukulia hatua wafanyabiashara

Picha
 MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wenye mitaji kuanzia sh. milioni 18 ambao hawatumii mashine za elektroniki (EFD’s) kama ilivyoagizwa na Serikali. Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Meneja wa TRA Mkoa, Peter Shewiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi kanda ya Ziwa. Shewiyo alisema hawatasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wataoshindwa kufuata kanuni na sharia ambazo zinawaelekeza kutumia mashine kwani kufanya hivyo kunakosesha serikali mapato. Alisema endapo wafanyabishara hao watatumia mashine hizo kutawezesha kuwapungazia wizi uliyopo katika kuongeza pato la taifa na kuwanufaisha wao wenyewe katika kutunza takwimu kwa usahihi. “Mfanyabiashara yeyote yule ambaye hatumii mashine za EFD’s haruhusiwi kufanya biashara na endapo tukimbaini mtu ambaye anaendesha biashara yake bila mashine hiyo, tutamshitaki pamoja na fidia,”alisema Shewiyo. Naye...

Malima ahimiza uwekezaji

Picha
SERIKALI imesema kuwa uchumi wa nchi hauwezi kukua bila ya kuwepo na uwekezaji wenye tija kwa taifa na jamii kwa ujumla. Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima wakati akifungua semina ya kujadili matokeo ya Afrika katika uchumi, iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa udhamini wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Alisema uwekezaji ndio unaosaidia kukuza uchumi wa taifa lolote duniani, hivyo bila ya kuwa na sekta binafsi zitakazoweza kuwekeza katika nyanja mbalimbali za maendeleo uchumi hautaweza kukua. “Unajua kuwa ukuaji mzuri wa uchumi unasukumwa na sekta binafsi na kama tunataka kuwa na maendeleo hapa kwetu ni lazima tuangalie ni njia gani zitumike ili uchumi unaokuwa uwanufaishe wananchi wote na si wachache. Ndio maana hawa wenzetu wa AfDB wametupatia fedha ili zitumike katika maeneo sita waliopendekeza wao ambayo wanadhani yanaweza kukuza zaidi uchumi wetu,” alisema. Malima aliyataja maeneo hayo sita kuwa ni uwongozi bora, ...

Sekta ya viwanda yachangia 3%

Picha
 TAKWIMU zinaonesha kwamba sekta ya viwanda katika pato la Taifa imekuwa kutoka asilimia 9.8 mwaka 2010 hadi kufika asilimia 10.2 mwaka 2012, sawa na ongezeko la asilimia 0.3. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Musa, alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya siku ya viwanda, inayoadhimishwa kila Novemba 20. Musa alisema pamoja na mafanikio hayo bado juhudi zinahitajika ili kuongeza uwekezaji hususani katika usindikaji wa bidhaa ili kuweza kukuza bidhaa hizo kwa masoko ya ndani na nje. Alizitaja njia zitakazosaidia kuleta mabadiliko  kuwa ni pamoja na kuhawilisha teknolojia na kuwezesha utafiti wa teknolojia zitakazosaidia katika kuongeza tija. Kuhusu maadhimisho ya siku ya viwanda, Musa alisema wameandaa maonesho ambayo yameanza jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere na yanatarajiwa kufika kilele chake Novemba 20 mwaka huu. Naye Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi kutoka Shirik...

Watanzania watakiwa kupima afya zao

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Seif Rashid, amewataka Watanzania kujijengea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara badala ya kusubiri wafikie dalili za ugonjwa hatua mbaya. Dk. Rashid, alisema hatua hiyo itawawezesha kupata matibabu mapema kabla ya kusababisha madhara makubwa. Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya afya kwa wabunge iliyoendeshwa na kituo cha afya cha Agakhan Bungeni jana, Dk. Rashid alisema kuwa watanzania wakijijengea tabia ya kupima wataepushwa na vifo visivyo vya lazima. "Magonjwa mengi yamekuwa yakianza taratibu, ndani kwa ndani, hivyo kama wananchi wakijenga tabia ya kupima afya angalau mara moja kwa mwezi na kupunguza kula vyakula ambavyo wataalamu wa afya wanakataza, itaepusha vifo vya ghafla vinavyotokea,” alisema na kuongeza. Tujitahidi kupunguza vyakula kama nyama choma, chumvi nyingi, itasaidia kuepusha matatizo yanayotukumba kama kisukari, shinikizo la damu na uzito kuzidi kupita kiwango cha urefu wa mtu. "Kumekuwa na tati...

Watanzania waaswa kuchangia elimu

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama, amesema watanzania wanapaswa kuondokana na dhana kuwa jukumu la kutoa elimu bora linapaswa kubebwa na serikali peke yake. Amesema dhana hiyo ndiyo huwaathiri kwa kiasi kikubwa watoto wa kike na kusababisha kushuka kwa kiwango chao cha elimu, baada ya kuhadaiwa na wanaume wakati wakitoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kutafuta elimu. Mhagama, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati akiwatunuku vyeti vya utambuzi wadau mbalimbali waliochangia ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto wa kike kupitia uhamasishaji uliofanywa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Alisema wananchi wamekuwa hodari kuchangia sherehe zinazotumia gharama kubwa huku wakishindwa kuhimizana kuchangia walau sh 200,000 katika kila kamati kwa ajili ya kuboresha mazingira ya elimu. “Wanaotunukiwa vyeti leo wamejijengea heshima kubwa katika sekta ya elimu kwa kuwa tupo zaidi ya milioni 40, lakini ni wachache waliojitokeza na hawa kwa nafa...

‘Acheni kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria za mazingira’

MAOFISA Mazingira katika Wilaya za mikoa ya Iringa na Mbeya wametakiwa kuacha kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria za uhifadhi wa mazingira. Kauli hiyo, imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi, wakati akifungua mafunzo ya siku  tano yaliyoshirikisha maofisa mazingira kutoka Wilaya 14 za mikoa hiyo, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Mushi, alisema kuwa wapo baadhi ya wawekezaji katika sekta za madini na nishati wasiozingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inayotaka shughuli yoyote ya maendeleo  kuendana na uhifadhi wa mazingira na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira. Alisema kuwa, maofisa mazingira wanatakiwa kusimamia  sheria za mazingira kwa kuhakikisha kuwa zinafuatwa, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wawekezaji wasiozingatia sheria hizo. Alisema kuwa katika sekta ya nishati, kuna shughuli za utafutaji  wa mafuta na gesi unaoendelea seh...