Ripoti ya Hoseah yavuruga Bunge

J Ndugai
 Sakata la uchotaji wa Dola za Marekani 200 milioni katika akaunti ya Tegeta Escrow limeendelea kuibuka kwa sura mbalimbali bungeni. Safari hii, Bunge limetakiwa kueleza ni kwa nini Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na

Kupambana na Rushwa (Takukuru) isifikishwe katika chombo hicho cha kutunga sheria sambamba na ile ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Hayo yalijitokeza bungeni jana baada ya wabunge kadhaa kusimamia wakitaka mwongozo wa Spika kuhusu uchunguzi huo, hasa kutokana na kuwapo taarifa kuwa ripoti ya CAG itawasilishwa bungeni mwishoni mwa mwezi huu, lakini ile ya Takukuru ambayo pia inachunguza suala hilo, haitapelekwa bungeni wala kujadiliwa.

Uchunguzi wa Akaunti ya Escrow uliamuliwa na Serikali baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kulipua ufisadi uliotokana na utata katika uchotaji wa fedha kwenye akaunti hiyo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina ya Shirika la Umeme

Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Katika mgogoro huo, Tanesco ilikuwa inabishia kiwango cha fedha ilichokuwa inalipa kwa gharama za uwekezaji kwa IPTL, ndipo ikaamuliwa na Mahakama ifunguliwe akaunti hiyo ili fedha ilizokuwa inalipa ziendelee kuwekwa huko hadi mgogoro utakapokwisha. Kesi hiyo iliamuliwa katika mazingira yanayoelezwa kuwa na utata na fedha hizo kuchukuliwa haraka na IPTL.

Jana, baada ya kipindi cha maswali na majibu, wabunge kadhaa walisimama wengi wakiwa wa upinzani wakitaka mwongozo kuhusu lini ripoti hizo mbili zitawasilishwa bungeni hasa baada ya ile ya Takukuru kuelezwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Dk Edward Hoseah kuwa imekamilika na kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji