RC, aipongeza Wilaya ya kibondo wa ujenzi Maabara
KIGOMA
RC, aipongeza Wilaya ya kibondo ujenzi Maabara
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa
Machibya ameupongeza uongozi wa wilaya ya kibondo na wananchi kwa ujumla juu ya kazi inayoendela
katika mikoa na wilaya zote hapa nchini ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari
Hayo ameyasema leo alipokuwa
akiongea kikao cha dharula cha baraza la
Baraza Halmashauri wilaya ya kakonko mkoani kigoma katika kuhamasisha
ujenzi wa maabara hizo,
Machibya amedema kuwa katika
wilaya zote za mkoa huo ni wilaya mbili tu ambazo zina uhakika wa kukamilisha
vizuri ujenzi huo mnamo November 30, 2014 ambazo ni Kigoma na Kibondo huku akizitupia lawama zingine kuwa baadhi yao
wamekuwa wakiwaachia wananchi peke yao kuwa waendelee na ujenzi na wataalam kutokufanya kazi zao inavyostaili
‘’ Jambo hili halitakubalika
kabisa nimekuta maeneo mengine wamejenga misingi ya tope kinyume na maelekezo
alisema Machibya’’
Aidha ameeleza kushangazwa na
kitendo cha wilaya ya kakonko kukutwa haijafanya maandalizi yoyote na kudai
kuwa ni lazima ujenzi huo ukamilike muda uliopangwa kwani maendeleo haya ni kwa
ajili ya watanzania wote hata kama serikali
ndo ina hamasisha na kuwataka viongozi
wakaige mfano wilaya jirani ya kibondo ambapo wao waka kwenye hatua nzuri za
ujenzi
Nae mkuu wa wilaya hiyo Piter
Toyima amemuhakikishia kuwa muda uliopangwa ujenzi huo utakuwa umekamilika na
kwa viwango vinavyotakiwa
Machibya alianza ziara ya
kukagua maendeleo ya ujenzi huo katika wilaya zote za mkoa wa kigoma ikiwa ni
Kasulu, Kibondo Buhigwe Uvinza Kigoma vijijini na Kakonko.
Maoni
Chapisha Maoni